Pars Today
Katibu wa Idara Kuu ya Misri inayohusika na Fatwa za Kiislamu (Darul Iftaa) amekosoa ombi lililowasilishwa na shakhsia 300 wa Ufaransa waliotaka kuondolewa baadhi ya aya katika kitabu kitakatifu cha Qur'ani.
Jumuiya ya International Action Group for Libya imezituhumu nchi za Imarati na Misri kuwa zinavuruga jitihada zinazofanywa na ujumbe wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya mapatano ya kitaifa nchini Libya.
Mahakama ya Misri imeweka idadi kubwa ya maafisa wa ngazi za juu wa Harakati ya Ikhwanul Muslimin katika orodha ya magaidi.
Sheikh Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kiislamu cha al-Azhar nchini Misri amesema kuwa, Beitul-Muqaddas ni ardhi ya Kiislamu na daima itaendelea kuubakia kuwa ni ya Kiislamu.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Sudan amewasilisha mashtaka ya nchi yake dhidi ya Misri kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa baada ya Misri kuendesha uchaguzi wa rais katika maeneo ya mpakani yanayogombaniwa ya Halaib na Shalateen.
Rais Abdul Fattah al-Sisi wa Misri ametangaza kurefusha muda wa hali ya hatari nchini humo kwa miezi mitatu mingine ambao ulianza kutekelezwa mwezi Aprili mwaka jana baada ya kujiri mashambulizi makubwa dhidi ya makanisa.
Shirika la kimataifa la haki za binadamu la Human Rights Watch limemtaka Rais Abdul Fattah el Sisi wa Misri kuhakikisha kuwa uvunjaji wa haki za binadamu unakomeshwa nchini mwake katika kipindi cha pili cha urais wake.
Jeshi la Misri linasema limewaua magaidi wane na kuwakamata wengine wengi katika oparesheni maalumu za kuwatimua magaidi walio katika eneo la Rasi ya Sinai.
Mkutano wa Misri, Sudan na Ethiopia wa kujadili suala tata la bwawa la al-Nahdha umegonga mwamba huku pande tatu hizo zikishindwa kuafikiana.
Rais Abdul Fattah al-Sisi ametangazwa mshindi wa kinyang'anyiro cha uchaguzi wa rais wa Misri baada ya kujipatia kura milioni 21 sawa na asilimia 97.08 ya kura zote na hivyo kupata ridhaa ya kuiongoza tena nchi hiyo kwa muhula wa pili.