Darul Iftaa ya Misri yakosoa ombi la shakhsia 300 wa Ufaransa
(last modified Wed, 25 Apr 2018 14:33:33 GMT )
Apr 25, 2018 14:33 UTC
  • Darul Iftaa ya Misri yakosoa ombi la shakhsia 300 wa Ufaransa

Katibu wa Idara Kuu ya Misri inayohusika na Fatwa za Kiislamu (Darul Iftaa) amekosoa ombi lililowasilishwa na shakhsia 300 wa Ufaransa waliotaka kuondolewa baadhi ya aya katika kitabu kitakatifu cha Qur'ani.

Khalid Omran amelitaja ombi hilo la raia hao 300 wa Ufaransa akiwemo Rais wa zamani wa nchi hiyo Nicolay Sarkozy kwa ajili ya kufutwa baadhi ya sura za Qur'ani Tukufu kuwa ni kitendo cha  uchupaji mipaka dhidi ya  Uislamu. Omran ameongeza kuwa shakhsia hao wa Ufaransa wamewasilisha ombi hilo katika kudhihirisha misimamo yao ya kufurutu ada ambayo imezilenga dini zote; misimamo ambayo inaiathiri pia dunia. 

Hakuna shaka kuwa shakhsia hao 300 wa nchini Ufaransa wakiwemo Rais wa zamani wa nchi hiyo Nicolay Sarkozy, Waziri Mkuu wa zamani Emmanuel Valls na shakhsia wengine wa kisiasa, kisanii na kiutamaduni wa nchini humo  wamewataka Waislamu kuzifuta sura katika Qur'ani Tukufu ambazo wamedai kuwa zinatoa wito wa kuuliwa na kuadhibiwa Mayahudi na Wakristo kupitia makala iliyochapishwa na gazeti la Le Parisien chini ya anwani "Hatua dhidi ya Uyahudi Mpya". 

Inafaa kuashiria hapa kuwa Waislamu nchini Ufaransa wamelaani vikali kitendo cha kuchapishwa makala hiyo  iliyovunjia heshima na kupotosha kitabu kitakatifu cha Qur'ani nchini humo.

Waislamu wa ufaransa wakiandamana kupinga makala hiyo ya upotoshaji kuhusu Qur'ani Tukufu 

Makala hiyo ya dharau na iliyo dhidi ya Uislamu ambayo imechapishwa hivi karibuni katika gazeti la Le Parisien mjini Paris, imesainiwa na rais wa zamani wa nchi hiyo, Nicolas Sarkozy, aliyekuwa waziri mkuu Manuel Valls na watu wengine 300.

Tags