Pars Today
Mtoto wa rais wa zamani wa Misri aliyeuzuliwa na kutiwa jela, amesema kuwa hali ya baba yake ni mbaya katika jela ya nchi hiyo na hakuna hatua zozote za maana zinazochukuliwa za kuhakikisha anapatiwa matibabu anayostahiki.
Ripoti zinaonesha kuwa, idadi kubwa ya vijana wa Misri hawakupiga kura katika uchaguzi wa rais wa nchi hiyo.
Rais Abdul Fattah al-Sisi wa Misri ameibuka mshindi wa uchaguzi tata wa rais uliofanyika Jumatatu iliyopita, kwa kuzoa asilimia 92 ya kura zote halali zilizopigwa.
Kamati moja ya bunge la Uingereza imefichua kuwa, kuna hatari ya kufariki dunia rais wa zamani wa Misri Mohammad Morsi kama serikali ya nchi hiyo haitoruhusu kupewa matibabu ya haraka.
Wamisri leo Jumatatu wameanza kupiga kura kumchagua Rais mpya katika uchaguzi wa rais usio na upinzani wa maana huku Abdel Fattah al Sisi akitazamiwa kuibuka mshindi baada ya serikali yake inayoungwa mkono na jeshi kuwafunga jela na kuwatisha wagombea wote wakuu waliokuwa wakitazamiwa kuchuana naye katika uchaguzi huu.
Assalaamu alaykum wapenzi wasikilizaji na karibuni katika sehemu nyingine ya mfulluizo huu wa Hadithi ya Uongofu.
Mashindano ya 25 ya kimataifa ya Qur'ani Tukufu yalianza jana Jumamosi tarehe 24 Machi, 2018 nchini Misri yakishirikisha wajumbe kutoka nchi 50 duniani.
Rais wa Sudan amesema kuwa nchi yake imedhamiria kwa dhati kutatua hitilafu zilizopo kati ya Khartoum na Cairo.
Uchaguzi wa rais wa Misri ulianza jana Ijumaa machi 16 kwa Wamisri wanaoishi katika nchi 124 za kigeni na utaendelea kwa muda wa siku tatu.
Uchaguzi wa rais wa Misri umenza leo Ijumaa nje ya nchi hiyo huku wapinzani wa serikali ya jenerali mstaafu, Abdul Fattah al Sisi wakiwataka wananchi wasusie zoezi hilo kwa hoja kwamba, halitakuwa huru na la wazi.