Uchaguzi wa rais Misri waanza nje ya nje, wapinzani wataka wananchi wasusie
Uchaguzi wa rais wa Misri umenza leo Ijumaa nje ya nchi hiyo huku wapinzani wa serikali ya jenerali mstaafu, Abdul Fattah al Sisi wakiwataka wananchi wasusie zoezi hilo kwa hoja kwamba, halitakuwa huru na la wazi.
Wamisri wanaoishi nje ya nchi hiyo wameamkia katika balozi wa nchi hiyo katika nchi 124 katika zoezi hilo litakaloendelea kwa kipindi cha siku tatu.
Rais wa Misri katika nchi kama Australia, Malaysia na New Zealand wameamkia katika balozi za nchi yao kwa ajili ya kuchagua mmoja kati ya wagombea wawili wa kiti cha rais ambao ni Abdul Fattah al Sisi na Mussa Mustafa Mussa.
Hata hivyo vinara wa vyama vya upinzani vilivyosusia uchaguzi huo wamewataka Wamisri wasishiriki katika zoezi hilo. Wanasiasa hao wanasema uchaguzi huo si huru na kwamba hauwezi kuwa wa haki na wa wazi.
Serikali ya Misri imewazuia wapinzani mashuhuri wa Rais Abdul Fattah al Sisi kushiriki katika uchaguzi huo kwa kutumia visingizio mbalimbali.
Wakati huo huo Ujerumani imetangaza kuwa haina imani na zoezi la uchaguzi wa rais nchini Misri na imeitaka serikali ya Cairo isitishe ukandamizaji wa wapinzani, jumuiya za kiraia na vyombo vya habari.
Uchaguzi wa rais ndani ya Misri utafanyika mwishoni mwa mwezi huu.