Pars Today
Shirika la Kimataifa la Msalaba Mwekundu limetangaza kuwa, wahajiri wapatao 44 ambao wengi wao ni kutoka nchi za magharibi mwa Afrika wamefariki dunia kwa kiu kaskazini mwa Niger baada ya lori walilokuwa wakisafiria kuharibika katikati ya jangwa.
Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa, raia milioni moja na laki tatu katika nchi ya Niger iliyoko magharibi mwa Afrika wamakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula.
Rais Mahamadou Issoufou wa Niger ametoa wito wa kuchukuliwa hatua madhubuti kwa ajili ya kukabiliana na ukosefu wa usalama na wakati huo huo kuungwa mkono suala la haki za binadamu barani Afrika.
Mlipuko wa homa ya manjano (Hepatitis E) umesababisha vifo vya makumi ya watu nchini Niger.
Jumuiya ya Wasomaji Bingwa wa Qur'ani na taasisi nyingine kadhaa zisizo za serikali nchini Niger zimetahadharisha kuhusu hali mbaya ya wakimbizi walioko katika maeneo ya kusini mashariki mwa nchi hiyo.
Jeshi la polisi la Nigeria limetangaza habari ya kuuawa watu wawili katika jimbo la Niger la katikati mwa nchi hiyo.
Serikali ya Niger imetangaza kuwa maafisa watatu wa polisi wametiwa nguvuni baada ya kuripotiwa kuwa walimshambulia mwandamanaji mmoja katika maandamano yaliyogeuka kuwa ya fujo ya wanachuo yaliyosababisha kifo cha mtu mmoja na kupelekea kufungwa chuo kikuu kikubwa zaidi cha nchi hiyo.
Afisa mmoja wa masuala ya usalama wa Niger alisema jana kwamba, wanamgambo 57 wa genge la kigaidi la Boko Haram waliuawa Jumapili usiku katika mapigano na wanajeshi wa serikali, kusini mashariki mwa nchi hiyo.
Mahakama ya Niger imewaachia huru watu 15 waliokuwa wakikabiliwa na tuhuma za kupanga jaribio la mapinduzi dhidi ya Rais Mahamadou Issoufou wa nchi hiyo.
Serikali za Uhispania, Ufaransa na Niger zimeunda muungano wa pamoja kwa ajili ya kupambana ipasavyo na kadhia ya wahajiri haramu na magendo ya binaadamu.