-
Jeshi la Nigeria laua Waislamu 10 wakishiriki Arubaini ya Imam Hussein AS
Oct 27, 2018 23:32Wanajeshi wa Nigeria wameushambulia msafara wa Waislamu wa madhehebu ya Shia waliokuwa wakishiriki katika maombolezo ya Arubaini ya Imam Hussein AS, viungani mwa mji mkuu wa nchi Abuja, na kuua shahidi kumi miongoni mwa waumini hao.
-
Nigeria yaweka amri ya kutotoka nje mjini Kaduna baada ya mapigano ya kikabila kuua watu 55
Oct 23, 2018 03:25Maafisa wa serikali ya Nigeria wametuma kikosi maalumu cha polisi katika jimbo la Kaduna la kaskazini mwa nchi hiyo na kutangaza amri ya masaa 24 ya kutotoka nje baada ya kutokea mapigano ya kikabila yaliyoua makumi ya watu.
-
Watu 55 wauawa katika mapigano ya kidini nchini Nigeria
Oct 21, 2018 10:18Watu wasiopungua 55 wameuawa katika mapigano ya kidini jimboni Kaduna, kaskazini magharibi mwa Nigeria.
-
Wakulima 12 wauawa na magaidi wa Boko Haram katika jimbo la Borno
Oct 21, 2018 04:14Kundi la kigaidi la Boko Haram limewaua wakulima wasiopungua 12 na kujeuhi makumi ya wengine, baada ya kufanya shambulio katika kitongoji kimoja katika mji wa Maiduguri ulioko katika jimbo la Borno kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.
-
UN: Kundi la wanamgambo la Nigeria lamewaachia watoto 833
Oct 12, 2018 13:31Kundi moja la wanamgambo ambalo linaendesha mapambano dhidi ya kundi la kigaidi la Boko Haram kaskazini mwa Nigeria limewaachia huru watoto 833 miongoni mwa ngazi zake.
-
Waziri wa zamani wa Nigeria na mfuatiliaji wa hatima ya mabinti wa Chibok kugombea urais
Oct 07, 2018 11:45Bi Obiageli Ezekwesili Waziri wa zamani wa Nigeria na mwasisi mwenza wa kundi linalofuatilia mahali walipo mabinti zaidi ya 200 waliotekwa nyara mwaka 2014 na kundi la kigaidi la Boko Haram leo ametangaza nia yake ya kuwania kiti cha urais mwakani.
-
Mamia ya Wanigeria wafanya tena maandamano mjini Abuja kutaka kuachiliwa huru Sheikh Zakzaky
Oct 06, 2018 11:36Waislamu nchini Nigeria wamefanya tena maandamano kulalamikia kuendelea kushikiliwa kiongozi wao Sheikh Ibrahim Zakzaky ambaye bado yuko jela licha ya Mahakama Kuu ya Nigeria kutoa amri ya kuchiliwa huru mwaka 2016.
-
Kundi la Boko Haram lashambulia kambi ya jeshi kaskazini mashariki mwa Nigeria
Sep 28, 2018 11:05Kundi la kigaidi la Boko Haram limefanya shambulio jingine dhidi ya kambi moja ya jeshi kaskazini mashariki mwa Nigeria.
-
Wafanyakazi wa umma Nigeria waanza mgomo wa nchi nzima
Sep 27, 2018 12:08Wanachama wa miungano mikuu ya wafanyakazi wa umma nchini Nigeria wameanza mgomo wa taifa zima leo Alkhamisi, baada ya mazungumzo kati yao na serikali kuhusu nyongeza ya kima cha chini cha mshahara kugonga mwamba.
-
Jeshi la Nigeria laua magaidi 14 wa Boko Haram na kuokoa raia 146 waliokuwa wametekwa nyara
Sep 25, 2018 10:41Askari wa jeshi la Nigeria wamewaua magaidi 14 wa kundi la Boko Haram katika operesheni inayolenga kutokomeza mabaki ya kundi hilo la kigaidi katika eneo la kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.