UN: Kundi la wanamgambo la Nigeria lamewaachia watoto 833
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i48747-un_kundi_la_wanamgambo_la_nigeria_lamewaachia_watoto_833
Kundi moja la wanamgambo ambalo linaendesha mapambano dhidi ya kundi la kigaidi la Boko Haram kaskazini mwa Nigeria limewaachia huru watoto 833 miongoni mwa ngazi zake.
(last modified 2026-02-21T22:51:18+00:00 )
Oct 12, 2018 13:31 UTC
  • UN: Kundi la wanamgambo  la Nigeria lamewaachia watoto 833

Kundi moja la wanamgambo ambalo linaendesha mapambano dhidi ya kundi la kigaidi la Boko Haram kaskazini mwa Nigeria limewaachia huru watoto 833 miongoni mwa ngazi zake.

Christophe Boulierac msemaji wa Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa (Unicef) amesema kuwa kundi hilo la wanamgambo la CJTF  liliundwa mwaka 2013 na vijikundi vya kiraia katika jimbo la Borno kwa lengo la kuendesha mapambano dhidi ya Boko Haram. Mwezi Septemba mwaka jana CJTF ilitia saini makubaliano ya kukomesha utumiaji watoto kama askari katika machafukoni nchini humo na kuwaachia watoto hao ambapo asilimia 40 miongoni mwao wana umri wa miaka 15 au chini yake. 

Christophe Boulierac, Msemaji wa Unicef 

Pernille Ironside Naibu Mwakilishi wa Unicef nchini Nigeria amesema kuwa hii ni hatua muhimu katika njia ya kuhitimisha utumiaji watoto vitani. Hata hivyo amesema bado kuna watoto wengine ambao wanatumika katika safu za makundi mengine ya wanamgambo ama katika medani ya vita au katika kazi za usaidizi.