-
Wapalestina 8 wauawa shahidi na jeshi la Israel katika maandamano ya Siku ya Ardhi
Mar 30, 2018 11:24Kwa akali Wapalestina wanane wameuawa shahidi na wanajeshi katili wa Israel katika maandamano ya Siku ya Ardhi, ya kulaani hatua ya utawala huo ghasibu ya kupora ardhi zao, yaliyofanyika leo karibu na uzio wa kibaguzi wa Israel katika Ukanda wa Gaza.
-
UNRWA: Wapalestina Ghaza wanakabiliwa na hali mbaya kibinadamu
Mar 29, 2018 02:06Kamishna Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuwahudumia Wakimbizi wa Palestina Bw. Pierre Krahenbuhl ameonya kuhusu kuendelea kuwa mbaya hali ya kibinadamu ya Wapalestina katika eneo la Ukanda wa Gaza ambalo liko chini ya mzingiro wa Utawala wa Kizayuni wa Israel.
-
Oman yahimiza kuungwa mkono haki za wananchi wa Palestina
Mar 28, 2018 11:48Waziri wa Mambo ya Nje wa Oman ameyahimiza mataifa ya dunia kuunga mkono haki za wananchi wa Palestina na mapambano yao hadi watakapopata ushindi na uhuru wao.
-
HAMAS: Vitisho vya Israel haviwezi kuzuia kufanyika maandamano ya haki ya kurejea makwao Wapalestina
Mar 28, 2018 02:43Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS imetangaza kuwa, vitisho vya utawala dhalimu wa Israel katu haviwezi kuzuia kufanyika maandamano makubwa ya haki ya kurejea makwao Wapalestina.
-
Jeshi la Israel lawateka nyara makumi ya Wapalestina
Mar 27, 2018 03:16Vikosi vya utawala wa Kizayuni vimewateka nyara makumi ya Wapalestina wakiwemo wanawake, katika eneo la Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan linalokaliwa kwa mabavu.
-
Ripoti: Facebook inahudumia malengo ya Israel
Mar 26, 2018 21:58Wizara ya Sheria ya Israel imetangaza kuwa, idara inayosimamia mtandao wa kijamii wa Facebook ilikubali asilimia karibu 85 ya matakwa ya utawala huo haramu ya kuondolewa na kuzuiwa maelezo yanayohusiana na Wapalestina na jinsi wanavyokandamizwa katika kurasa za mtandao huo.
-
Palestina yakaribisha maazimio ya UN dhidi ya utawala wa Kizayuni
Mar 25, 2018 23:49Msemaji wa serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Palestina amekaribisha kupasishwa katika Umoja wa Mataifa maazimio matano ya haki za binadamu dhidi ya utawala wa Kizayuni.
-
Israel imebomoa nyumba elfu tano za Wapalestina katika mji wa Baitul Muqaddas
Mar 15, 2018 03:50Ripoti mpya iliyotolewa na Kituo cha Utafiti wa Ardhi (LRC) cha Palestina inaonyesha kuwa utawala haramu wa Kizayuni wa Israel umebomoa nyumba zipatazo 5,000 za Wapalestina katika mji wa Baitul Muqaddas (Jerusalem) tangu ulipouvamia na kuanza kuukalia kwa mabavu mji huo mwaka 1967.
-
Wapalestina wasusia mkutano wa White House, Israel na Waarabu kuhusu Gaza
Mar 14, 2018 10:47Mamlaka ya Ndani ya Palestina imekataa kushiriki mkutano uliofanyika katika Ikulu ya Marekani ya White House, na kuwaleta pamoja viongozi wa nchi za Kiarabu na utawala wa Kizayuni wa Israel.
-
Hizbullah ya Lebanon: Quds itabakia milele kuwa mji mkuu wa Palestina
Mar 14, 2018 00:05Naibu Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon amesisitiza kuwa njia ya ufumbuzi wa kadhia ya Palestina haiko mikononi mwa Marekani, bali kinachopasa kufanywa ni kuzifuatilia jinai zinazotendwa na Marekani.