Bendera ya Palestina yapepea katika kilele cha Mlima Kilimanjaro
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i43070-bendera_ya_palestina_yapepea_katika_kilele_cha_mlima_kilimanjaro
Kikundi cha mabinti na vijana 16 wa Kipalestina kimefanikiwa kufika katika kilele cha Mlima Kilimanjaro nchini Tanzania na kupeperusha bendera ya Palestina katika mlima huo mrefu zaidi barani Afrika.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Apr 13, 2018 23:25 UTC
  • Bendera ya Palestina yapepea katika kilele cha Mlima Kilimanjaro

Kikundi cha mabinti na vijana 16 wa Kipalestina kimefanikiwa kufika katika kilele cha Mlima Kilimanjaro nchini Tanzania na kupeperusha bendera ya Palestina katika mlima huo mrefu zaidi barani Afrika.

Vijana hao wa Kipalestina wakiwa wamebeba jumbe mbalimbali kama amani na matumaini kwa wagonjwa wa maradhi ya kansa wamesema kuwa, wamefanikiwa kufika katika kilele cha Mlima Kilimanjaro baada ya kuvumilia taabu na mashaka mengi hasa ya hakli ya hewa.

Majeda Subhi mama wa Duaa Subhi mmoja wa mabinti na vijana 16 wa Kipalestina waliofika katika kilele cha Mlima Kilimanjaro  ameandika katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Facebook kwamba, kikundi hicho kimefika juu ya mlima huo baada ya safari yya siku tano iliyoambatana na magumu mengi kama changamoto yya hali ya hewa.

Wapanda mlima wa Kipalestina wakiwa vkatika kituo cha mwisho katika kilele cha Mlima Kilimanjaro

Jarrah al-Hawamda, mmoja wa mabinti hao wa Kipalestina aliyefanikiwa kufika kkatika kilele cha Mlima Kilimanjaro na kutundika bendera ya Palestina alikuwa amebeba ujumbea wa matumaini kwa wagonjwa wa maradhi ya kansa uliokuwa unasema: "Hakuna kitu ambacho hakiwezekani katika ulimwengu huu".

Mlima Kilimanjaro ndio mlima mrefu kuliko yote Afrika, pia ni wa pili kwa urefu duniani. Mlima huu uko nchini Tanzania katika Mkoa wa Kilimanjaro. Una urefu wa futi 19,340 (mita 5,895).

Zaidi ya watalii 20,000 hupanda mlima huu kila mwaka wakiwemo wageni kutoka nje ya Tanzania na Watanzania. Mpandaji wa mlima huu huhitaji angalau siku tano, siku tatu kupanda na siku mbili kuteremka.