Pars Today
Mwakilishi wa Qatar katika Umoja wa Mataifa amewasilisha mashitaka kwa Baraza la Usalama la Umoja dhidi ya Imarati kutokana na hatua yake ya kichokozi ya kukiuka anga yake.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Qatar amesema kuwa, lau ingelitaka, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ingeliweza kutumia tofauti zake za kisiasa na Doha kuwatesa kwa njaa wananchi wa Qatar, lakini kamwe haikufanya hivyo.
Qatar imesema kukatwa uhusiano wa kidiplomasia, mzingiro na vikwazo ilivyowekewa na Saudi Arabia na waitifaki wake ni vita vya kiuchumi na Doha ipo mbioni kuhakikisha kuwa inafidiwa kutokana na hatua hizo za kiuhasama.
Katika kile kinachoonekana ni kukosekana matumaini kabisa ya kutatuliwa mgogoro ulioanzishwa na Bani Saud dhidi ya Qatar, serikali ya kifalme ya Saudi Arabia imeamua kuufunga kikamilifu kivuko cha mpaka wake wa ardhini na Qatar ambacho ilikifungua kidogo wakati wa msimu wa Hija.
Serikali ya Uturuki imekasirishwa sana na hatua ya waziri wa mambo ya nje wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) aliyetuma ujumbe kwenye ukurasa wake wa Twitter na kumtuhumu Rais Recep Tayyip Erdogan kuwa ni kutoka kizazi cha Waturuki waliofanya wizi mjini Madina na kukandamiza Waarabu wakati wa utawala wa Uthmaniyyah (Ottoman Empire).
Waziri wa Mambo ya Nje wa Umoja wa Falme za Kiarabu ameeleza kughadhibishwa kwa Imarati na hatua ya shirika moja la kutetea haki za binadamu kufungua faili la jinai za kivita za nchi hiyo dhidi ya Yemen.
Afisa mwandamizi wa usalama wa Umoja wa Falme za Kiarabu ametoa mwito kwa muungano wa kijeshi wa Saudi Arabia kuishambulia kwa bomu kanali ya televisheni ya al-Jazeera ya Qatar.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Qatar amekosoa vikali sera ya utawala wa Aal-Saud ya kuwakandamiza wananchi wa Saudi Arabia na wakati huo huo kuzichochea nchi nyingine.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Qatar ameutaja uhusiano uliopo kati ya nchi yake na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuwa wa "kipekee".
Waziri wa Mambo ya Nje wa Qatar amesema utawala wa Saudi Arabia unachochea migogoro na mivutano katika eneo la Mashariki ya Kati sambamba na kuzikandamiza na kuzinyanyasa nchi ndogo katika eneo ili kuzishinikiza zipige magoti mbele yake.