-
Mufti Mkuu wa Oman aunga mkono kususiwa utawala haramu wa Israel
Dec 31, 2022 05:40Mufti Mkuu wa Oman ameunga mkono mpango wa Bunge la nchi hiyo wa kususiwa utawala haramu wa Israel unaotenda jinai kila uchao huko Palestina.
-
Hizbullah yaipongeza timu ya soka ya Morocco kwa kuinyuka Uhispania na kuinua bendera ya Palestina
Dec 07, 2022 10:22Naibu Katibu Mkuu wa harakati ya Hizbullah ya Lebanon, Sheikh Naim Qassem ametuma ujumbe kwenye mtandao wa kijamii wa "Twitter" ambapo ameipongeza Morocco kwa ushindi wa timu ya kandanda ya nchi hiyo dhidi ya Uhispania hiyo jana na kufuzu kuingia robo fainali ya mechi za Kombe la Dunia zinazoendelea nchini Qatar.
-
Al Jazeera yawasilisha mashtaka ya mauaji Shireen kwenye mahakama ya kimataifa ya ICC
Dec 06, 2022 23:43Mtandao wa Habari wa Al -Jazeera umetangaza kuwa umewasilisha kesi ya mauaji ya mfanyakazi wake, Shireen Abu Akleh, katika Mahakama ya Jinai ya Kimataifa huko Hague.
-
Ripoti: Harakati ya kutetea ushoga iliibua tatizo kubwa ndani ya timu ya taifa ya Ujerumani huko Qatar
Dec 06, 2022 23:42Harakati ya "kuziba midomo" iliyofanywa na wachezaji wa timu ya taifa ya mpira wa miguu ya Ujerumani kwenye mechi yao ya ufunguzi katika Kombe la Dunia 2022 huko Qatar dhidi ya Japan, ilisababisha matatizo ndani ya kambi ya timu hiyo, na kuibua tofauti kati ya wachezaji ambao walikataa kushiriki kwenye kampeni ya kutetea ushoga.
-
Njama ya UAE yazimwa na "kampeni ya kufelisha uanzishaji uhusiano na Israel"
Dec 05, 2022 08:36Kuzinduliwa kampeni kwenye mitandao ya kijamii yenye alama ya hashtag "Kufeli Uanzishaji Uhusiano na Israel Katika Kombe la Dunia Qatar" kumekaribishwa kwa wingi na wanaharakati wa Muungano wa Falme za Kiarabu, Imarati na nchi zingine za Kiarabu ambao wote wamesisitiza kwa kauli moja kwamba, Kombe la Dunia la Soka nchini Qatar limefichua na kuzima njama ya Imarati ya kueneza mpango wa kuanzisha uhusiano na Wzayuni.
-
Kombe la Dunia, Iran yaipongeza Qatar, yasisitiza kuimarishwa uhusiano wa pande zote
Nov 28, 2022 23:49Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameipongeza Qatar kwa kuendesha vizuri mashindano ya Kombe la Dunia la mpira wa miguu 2022 na kusisitizia wajibu wa kuimarishwa uhusiano wa Tehran na Doha katika nyuga zote.
-
Takriban watu 900 walisilimu pambizoni mwa Kombe la Dunia, Qatar
Nov 27, 2022 04:21Hadi sasa watu 887 kutoka nchi tofauti wamesilimu kando ya Kombe la Dunia la mwaka huu wa 2022.
-
Mashabiki wa soka waendelea kuiunga mkono Palestina katika Kombe la Dunia
Nov 24, 2022 04:02Mashabiki wa soka wanaoshuhudia fainalii za mashindano ya kandanda ya Kombe la Dunia nchini Qatar wameendelea kuonyesha himaya na uungaji mkono wao kwa taifa la Palestina.
-
Kombe la Dunia; Vijana wa Kiarabu wakataa kuzungumza na wanahabari wa Israel
Nov 21, 2022 07:55Mashabiki wa soka wa nchi za Kiarabu wamekataa kuzungumza na waandishi wa habari wa mashirika ya utawala haramu wa Israel nchini Qatar, kunakofanyika fainali za Kombe la Dunia za mwaka huu 2022; kuonyesha upinzani wao wa kuanzishwa uhusiano wa kawaida na utawala huo bandia unaokalia kwa mabavu ardhi za Palestina.
-
Rais wa FIFA: Hakuna pombe viwanjani wakati wa Kombe la Dunia
Nov 19, 2022 23:14Rais wa Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) amepuulizia mbali mashinikizo ya kutaka kuruhusiwa pombe viwanjani wakati wa fainali za Kombe la Dunia zinazoanza leo nchini Qatar.