Mashabiki wa soka waendelea kuiunga mkono Palestina katika Kombe la Dunia
(last modified Thu, 24 Nov 2022 07:32:59 GMT )
Nov 24, 2022 07:32 UTC
  • Mashabiki wa soka waendelea kuiunga mkono Palestina katika Kombe la Dunia

Mashabiki wa soka wanaoshuhudia fainalii za mashindano ya kandanda ya Kombe la Dunia nchini Qatar wameendelea kuonyesha himaya na uungaji mkono wao kwa taifa la Palestina.

Mashabiki wa soka wa mataifa mbalimbali wameonekana wakiingia viwanjani kushuhudia mechi mbalimbali za Kombe la Dunia zinazoendelea nchini Qatar wakiwa wamebeba bendera ya Palestina.

Katika mechi iliyochezwa jana ya kundi F baina ya Morocco na Croatia na kumalizika kwa sare ya tasa, baadhi ya mashabiki na watazamaji wa mechi hiyo walioeneka wakiwa wamebeba bendera kubwa ya Palestina na kutangaza himaya na uungaji mkono wao kwa taifa madhulumu la Palestina.

Baadhi ya watazamaji walikuwa wamebeba vitambaa na maberamu yaliyoandikwa maandishi na jumbe za kuonyesha kupinga kuanzishwa uhusiano wa kawaida na utawala ghasibu wa Israel.

 

Hayo yanajiri katika hali ambayo, matukio ya baadhi ya mashambiiki wa soka wa mataifa ya Kiislamu na Kiarabu ya kukataa na kuvisusia vyombo vya habari vya Israel huko Qatar imewawakasirisha sana Wazayuni hasa baada ya kuona Palestina inaendelea kuungwa mkono kila mahali hata katika mashindano ya sasa Kombe la Dunia huko nchini Qatar.

Baadhi ya mashambiki hao wanapohojiwa na vyombo vya habari na mwanadishi kujitambulisha kwamba wanatoka katika chombo fulani cha habari cha Israel hukataa kufanya mahojiano na kumueleza mwandishi huyo kwamba, hakuna nchi inayojulikana kwa jina la Israel bali ni ardhi za Palestina zilizokabiliwa kwa mabavu na kupachikwa jina bandia la Israel.

Vyombo vya habari vya Israel vimeripoti kuwa, vijana wa Lebanon, Qatar na Saudi Arabia miongoni mwa nchi nyingine za Kiarabu walioko Qatar wamekataa kuhojiwa na wanahabari wa kanali ya 12 ya Kizayuni.