-
Jordan kumuita balozi wake wa Romania kupinga hatua ya nchi hiyo dhidi ya Quds
Apr 18, 2019 03:59Jordan imesema kuwa itamuita nyumbani balozi wake wa Romania, ikiwa ni jibu kwa hatua ya nchi hiyo ya Ulaya kutangaza kuwa itauhamishia ubalozi wake katika mji wa Quds, huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu kutoka Tel Aviv.
-
Rais wa Lebanon: Tangazo la Trump kuhusu miinuko ya Golan na Quds ni kinyume na maazimo ya kimataifa
Apr 12, 2019 04:25Rais Michel Aoun wa Lebanon kwa mara nyingine tena amesisitiza kuwa, tangazo la Rais Donald Trump wa Marekani kuhusiana na umiliki wa utawala vamizi wa Israel kwa miinuko ya Golan ya Syria linakinzana na maazimio ya kimataifa.
-
Rouhani: Quds ni mji mkuu wa kudumu wa Palestina na Golan haiwezi kutenganishwa na Syria
Apr 07, 2019 02:28Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa, Quds ni mji mkuu wa kudumu wa Palestina na miinuko ya Golan ni ardhi ya Syria isiyotenganishika na ardhi nyingine za nchi hiyo na kwamba hatua yoyote iliyo kinyume na hivyo ni kukanyaga maamuzi wa Umoja wa Mataifa na ni kinyume na uhakika wa kihistoria.
-
Idadi ya wanajeshi wa Israel walioangamizwa kaskazini mwa Quds imeongezeka
Mar 18, 2019 14:26Vyombo vya habari vya Kizayuni leo Jumatatu vimetangaza kuwa kuhani mmoja wa Kizayuni ambaye alijeruhiwa katika oparesheni ya kijana wa Kipalestina karibu na kitongoji cha Ariel kaskazinii mwa mji wa Salfit katika Ukingo wa Magharibi mwa Mto Jordan ameaga dunia.
-
Matakwa matatu ya Kamisheni ya Masuala ya Palestina ya Bunge la Jordan dhidi ya Israel
Mar 15, 2019 07:21Kamisheni ya Masuala ya Palestina ya Bunge la Jordan imetoa wito wa kufukuzwa balozi wa Israel mjini Amman, kurejeshwa nyumbani balozi wa Jordan huko katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu na kufutwa mkataba wa gesi na Israel.
-
Spika wa Bunge la Lebanon: Eneo lote la Quds ni mji mkuu wa Palestina
Mar 12, 2019 02:54Spika wa Bunge la Lebanon kwa mara nyingine tena amesisitiza msimamo wa nchi yake kuhusiana na kuiunga mkono Baytul -Muqaddas na Palestina na kusema kuwa, eneo lote la Quds Tukufu ni mji mkuu wa nchi ya Palestina.
-
Wazayuni wawatia nguvuni wasimamizi wa Matukufu ya Kiislamu Quds
Feb 24, 2019 14:19Polisi ya utawala haramu wa Israel imewakamata wasimamizi wa ngazi za juu wa Matukufu ya Kiislamu katika mji mtukufu wa Quds, huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu.
-
Miaka 40 na juhudi za kuunganisha madhehebu za Kiislamu
Feb 02, 2019 04:35Katika mada ya 11 ya Katiba ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kwa msingi wa Aya ya Qur'ani Tukufu inayosema: Hakika umma wenu huu ni umma mmoja, na Mimi ni Mola wenu, kwa hivyo niabuduni Mimi, serikali ya Jamhuri ya Kiislamu inawajibika kuratibu siasa zake kuu kwa msingi wa kuleta umoja na mshikamano wa kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni kati ya mataifa yote ya Kiislamu.
-
UN yapinga vikali mashambulizi ya Wazayuni wa Israel huko Quds
Jan 28, 2019 07:36Nickolay Mladinov ambaye ni mjumbe maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika eneo la Mashariki ya Kati amesema kuwa mashambulizi ya walowezi wa Kizayuni dhidi ya kijiji cha kaskazini mwa Quds (Jerusalem) hayakubaliki na yanashtua sana.
-
Utawala wa Kizayuni unapanga njama ya kuzima sauti ya adhana Baitul Muqaddas Mashariki
Jan 03, 2019 03:11Televisheni ya utawala wa Kizayuni wa Israel imetangaza kuwa manispaa ya utawala huo haramu katika eneo la Baitul Muqaddas Mashariki (East Jerusalem) ina mpango wa kuzuia sauti ya adhana isisikike katika misikiti ya eneo hilo la Palestina inayokaliwa kwa mabavu.