-
Maelfu waandamana Zimbabwe kumuunga mkono Mugabe
May 25, 2016 10:02Maelfu ya wananchi wa Zimbabwe wamejitokeza barabarani katika mji mkuu Harare, kushiriki maandamano ya kuonyesha uungaji mkono wao kwa rais wa nchi hiyo, Robert Mugabe, mwenye umri wa miaka 92.
-
Mahakama ya Katiba Comoro yaidhinisha ushindi wa Kamanda Azali Assoumani
May 15, 2016 23:08Mahakama ya Katiba nchini Comoro imemtangaza Kamanda Azali Assoumani kuwa mshindi wa duru ya pili ya uchaguzi wa rais katika visiwa hivyo.
-
Rais wa Guinea-Bissau amfuta kazi Waziri Mkuu na kuvunja serikali
May 13, 2016 03:39Rais José Mário Vaz wa Guinea-Bissau amempiga kalamu Carlos Correia, Waziri Mkuu wa nchi hiyo na kutangaza kuivunja serikali.
-
Besigye kuendelea kuzuiliwa wakati Rais Museveni wa Uganda akiapishwa
May 12, 2016 03:32Katika hali ambayo Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda anatazamiwa kuapishwa wakati wowote tokeo sasa, kinara wa upinzanai nchini humo Dakta Kizza Besigye anaendelea kuzuiliwa katika jela ya Nalufenya wilayani Jinja eneo la Karamoja.
-
Mgombea urais wa wapinzani Kongo aitwa mahakamani
May 08, 2016 03:09Mwendesha mashtaka mkuu wa mji wa Lubumbashi, kusini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo amemwita mahakamani mgombea wa urais wa muungano wa wapinzani.
-
Rais wa Equitorial Guinea ahifadhi kiti chake kwa kupata 98% ya kura
Apr 26, 2016 03:53Matokeo ya awali ya uchaguzi mkuu nchini Equitorial Guinea yanaonyesha kuwa Rais Teodoro Obiang Nguema ameshinda kiti hicho kwa kupata asilimia 98 ya kura zilizopigwa.
-
Riek Machar kuwasili Juba leo kuunda serikali na Salva Kiir
Apr 18, 2016 23:24Kiongozi wa upinzani wa Sudan Kusini anatazamiwa kuwasili katika mji mkuu wa nchi hiyo Juba hii leo, kwa shabaha ya kuunda serikali ya umoja wa kitaifa akishirikiana na Rais Salva Kiir wa nchi hiyo.
-
Shein ateua baraza la mawaziri, asema hatishwi na 'kelele' za CUF
Apr 10, 2016 03:26Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dakta Ali Mohamed Shein ametangaza Baraza la Mawaziri lenye wizara 13 huku akisema kuwa hababaishwi na hatua ya chama kikuu cha upinzani visiwani humo CUF kutoitambua serikali yake.
-
Upinzani Djibouti: Kulikuwa na udanganyifu kwenye uchaguzi wa rais
Apr 10, 2016 03:21Viongozi wa upinzani nchini Djibouti wametangaza kutotambua ushindi wa Rais Ismail Omar Guelleh katika uchaguzi mkuu uliofanyika Ijumaa iliyopita.
-
Uchaguzi wa rais Djibouti, baadhi ya wakuu wa upinzani waususia
Apr 08, 2016 04:36Wananchi wa Djibouti waliotimiza mashari ya kupiga kura leo wameelekea kwenye masanduku ya kupiga kura kumchagua rais mpya, katika uchaguzi ambao aghalabu ya vyama vya upinzani nchini humo vimeususia.