Uchaguzi wa rais Djibouti, baadhi ya wakuu wa upinzani waususia
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i4654-uchaguzi_wa_rais_djibouti_baadhi_ya_wakuu_wa_upinzani_waususia
Wananchi wa Djibouti waliotimiza mashari ya kupiga kura leo wameelekea kwenye masanduku ya kupiga kura kumchagua rais mpya, katika uchaguzi ambao aghalabu ya vyama vya upinzani nchini humo vimeususia.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Apr 08, 2016 04:36 UTC
  • Uchaguzi wa rais Djibouti, baadhi ya wakuu wa upinzani waususia

Wananchi wa Djibouti waliotimiza mashari ya kupiga kura leo wameelekea kwenye masanduku ya kupiga kura kumchagua rais mpya, katika uchaguzi ambao aghalabu ya vyama vya upinzani nchini humo vimeususia.

Hatua hiyo imemuandalia rais wa sasa Ismail Omar Guelleh mazingira ya kuhifadhi kiti hicho ambacho anakikalia tangu mwaka 1999.

Wagombea 6 wa upinzani wanatazamiwa kujitosa kwenye kinyang'anyoro hicho lakini wanaotazamiwa kutoa ushindani mkubwa dhidi ya Rais Guelleh ni Omar Elmi Kaireh na Mohamed Daoud Chehem.

Kwa mujibu wa Tume ya Uchaguzi ya Djibouti, wapiga kura zaidi ya laki moja na 80 elfu wanatazamiwa kushiriki zoezi hilo na kwamba matokeo ya uchaguzi huo yanatazamiwa kutolewa kufikia leo jioni.

Djibouti ambayo ni nchi ndogo ya Pembe ya Afrika yenye idadi ya watu wasiofikia hata milioni moja, mwaka 2011 ilishuhudia wimbi la maandamano ya kupinga kuchaguliwa tena Rais Guelleh ambaye ilisemakana kuwa alipata asilimia 80 ya kura zilizopigwa. Iliarifiwa kuwa serikali ilitumia mkono wa chuma kuwakandamiza wapinzani waliokuwa wakitaka Rais Ismail Omar Guelleh anayeshikilia wadhifa huo tangu mwaka 1999 ang'oke madarakani.

Maandamano hayo yalijiri baada ya Rais Guelleh kuifanya marekebisho katiba ya nchi, ili kumruhusu kugombea kiti hicho kwa mara ya tatu mfululizo.

Baada ya kula kiapo cha kulitumikia taifa mwaka 2011, Omar Guelleh aliapa kwamba hatagombea tena kiti cha rais mwaka huu wa 2016.