-
India kuwafukuza wakimbizi Waislamu wa Myanmar wapatao 40,000
Sep 17, 2017 03:07Serikali ya India imewasilisha ombi katika Mahakama ya Juu ya nchi hiyo la kutaka kutimuliwa makumi ya maelfu ya wakimbizi Waislamu wa kabila la Rohingya, waliokimbilia usalama wao nchini humo kutokana na kushadidi mashambulizi ya jeshi la Myanmar likishirikiana na Mabudha wenye misimamo mikali dhidi yao.
-
Watafiti: Waislamu wa Rohingya waliofanikiwa kufika Bangladesh wanasumbuliwa na matatizo ya kisaikolojia
Sep 15, 2017 09:39Wafanyakazi wa misaada ya kibinaadamu nchini Bangladesh wameviambia vyombo vya habari kwamba Waislamu wa Rohingya waliofanikiwa kufika nchini humo, wanasumbuliwa na matatizo ya kisaikolojia kutokana na mateso ya kimwili waliyoyashuhudia nchini Myanmar kutoka kwa askari wa serikali ya nchi hiyo.
-
FAO: Waislamu laki moja Warohingya walioko Bangladesh wanahitajia msaada wa haraka wa chakula
Sep 15, 2017 00:03Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) limetangaza kuwa, Waislamu laki moja wa jamii ya Rohingya waliowasili nchini Bangladesh wanahitajia msaada wa haraka wa chakula.
-
UN yaeleza wasi wasi wake kuhusu wimbi la wakimbizi wa Rohingya nchini Bangladesh
Sep 09, 2017 03:15Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR limeeleza wasi wasi mkubwa lilionao kutokana na kuendelea kumiminika idadi kubwa ya wakimbizi Waislamu wa jamii ya Rohingya nchini Bangladesh.
-
Desmond Tutu amtaka San Suu Kyi kukomesha mauaji ya Waislamu Myanmar
Sep 09, 2017 00:01Askofu Mkuu wa Afrika Kusini, Desmond Tutu amemtaka Mshauri Mkuu wa Serikali ya Myanmar na mshindi mwenzake wa Tuzo ya Amani ya Nobel, Aung San Suu Kyi kukomesha mauaji yanayofanywa na jeshi la nchi hiyo dhidi ya Waislamu wa jamii ya Rohingya.
-
ISESCO yataka Aung San Suu Kyi anyang'anywe tuzo ya Nobel, Waislamu waendelea kuuawa Myanmar
Sep 06, 2017 07:42Shirika la Elimu, Sayansi na Utamasdu la Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (ISESCO) limetangaza kuwa, Mshauri Mkuu wa Serikali ya Myanmar, Aung San Suu Kyi anapaswa kunyang'anywa Tuzo ya Amani ya Nobel kutokana na mauaji ya kutisha yanayoendelea kufanyika nchini humo dhidi ya Waislamu.
-
BHRN: Sio Waislamu wa Rakhine tu wanaouawa Myanmar
Sep 05, 2017 23:19Shirika moja la kutetea haki za binadamu nchini Myanmar limetoa ripoti iliyofichua kuwa Waislamu katika maeneo yote ya nchi hiyo wanauawa na kuhujumiwa na wanajeshi wa nchi hiyo na sio wa kabila la Rohingya tu katika mkoa wa Rakhine.
-
Israel yashirikiana kijeshi na Mynamar inayoua kikatili Waislamu
Sep 04, 2017 11:52Huku utawala wa mabudha wa Myanmar ukiendeleza ukatili wake dhidi ya Waislamu wa Rohingya, utawala wa Kizayuni wa Israel unaowakandamiza kikatili Waislamu wa Palestina nao unaimarisha ushirikiano wake wa kijeshi na serikali ya Myanmar.
-
Waislamu Indonesia waandamana kuwatetea wenzao wa Rohingya
Sep 02, 2017 23:24Waislamu nchini Indonesia wamejitokeza kwa wingi mabarabarani kushiriki maandamano ya kulaani mauaji na jinai wanazofanyiwa Waislamu wenzao wa kabila la Rohingya huko Myanmar.
-
Jamii ya kimataifa yatakiwa kuvunja kimya chake mbele ya mauaji ya Waislamu Myanmar
Aug 31, 2017 23:44Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kutetea Haki za Waislamu wa jamii ya Rohingya yenye makao yake nchini Uingereza amekosoa vikali kimya cha jamii ya kimataifa mbele ya mauaji yanayoendelea kufanywa na Mabudha wenye misimamo mikali dhidi ya Waisalmu nchini Myanmar