BHRN: Sio Waislamu wa Rakhine tu wanaouawa Myanmar
https://parstoday.ir/sw/news/world-i33961-bhrn_sio_waislamu_wa_rakhine_tu_wanaouawa_myanmar
Shirika moja la kutetea haki za binadamu nchini Myanmar limetoa ripoti iliyofichua kuwa Waislamu katika maeneo yote ya nchi hiyo wanauawa na kuhujumiwa na wanajeshi wa nchi hiyo na sio wa kabila la Rohingya tu katika mkoa wa Rakhine.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Sep 06, 2017 03:49 UTC
  • BHRN: Sio Waislamu wa Rakhine tu wanaouawa Myanmar

Shirika moja la kutetea haki za binadamu nchini Myanmar limetoa ripoti iliyofichua kuwa Waislamu katika maeneo yote ya nchi hiyo wanauawa na kuhujumiwa na wanajeshi wa nchi hiyo na sio wa kabila la Rohingya tu katika mkoa wa Rakhine.

Ripoti iliyotolewa jana Jumanne na Burma Human Rights Network imesema kuwa, serikali inawaunga mkono wanajeshi na mabudha wenye misimamo mikali kuwashambulia Waislamu katika kila pembe ya nchi hiyo ya mashariki mwa bara Asia.

Ripoti hiyo imesema kuwa, mbali na Waislamu wa Myanmar kunyimwa huduma za msingi kama matibabu wanapokwenda hospitalini, lakini pia serikali imekataa katakata kuwapa vitambulisho vya taifa.

Ripoti ya Burma Human Rights Network imebainisha kuwa, Waislamu katika miji na vijiji 46 nchini Myanmar wanapitia kila aina ya jinai kutoka kwa askari wa jeshi la nchi hiyo wakishirikiana na Mabudha wenye misimamo mikali.

Mabudha wa Myanmar wanaoua Waislamu kwa msaada wa serikali

Tangu tarehe 25 Agosti mwaka huu, jeshi la Myanmar kwa kushirikiana na Mabudha wenye misimamo mikali limekuwa likiwashambulia Waislamu wa jimbo la Rakhine, ambapo zaidi ya 400 miongoni mwao wamekwishauawa, huku wengine zaidi ya laki 1 na 25 elfu wakikimbilia Bagladesh.

Mauaji na jinai hizi zinafanyika mkabala wa kimya cha taasisi husika za kimataifa kama vile Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.