Israel yashirikiana kijeshi na Mynamar inayoua kikatili Waislamu
https://parstoday.ir/sw/news/world-i33928-israel_yashirikiana_kijeshi_na_mynamar_inayoua_kikatili_waislamu
Huku utawala wa mabudha wa Myanmar ukiendeleza ukatili wake dhidi ya Waislamu wa Rohingya, utawala wa Kizayuni wa Israel unaowakandamiza kikatili Waislamu wa Palestina nao unaimarisha ushirikiano wake wa kijeshi na serikali ya Myanmar.
(last modified 2026-01-14T08:12:18+00:00 )
Sep 04, 2017 11:52 UTC
  • Israel yashirikiana kijeshi na Mynamar inayoua kikatili Waislamu

Huku utawala wa mabudha wa Myanmar ukiendeleza ukatili wake dhidi ya Waislamu wa Rohingya, utawala wa Kizayuni wa Israel unaowakandamiza kikatili Waislamu wa Palestina nao unaimarisha ushirikiano wake wa kijeshi na serikali ya Myanmar.

Gazeti la Haaretz la utawala wa Kizayuni limeripoti leo (Jumatatu) kuwa katika ziara ya mwaka jana ya nchini Myanmar ya Michel Ben-Baruch, mkuu wa kitengo cha utawala wa Kizayuni cha kusafirisha nje vifaa vya kijeshi, utawala wa Kizayuni ulikubaliana na nchi hiyo kuiuzia boti za kisasa za kivita.

Wahanga wakuu wa ukatili wa mabudha wa Myanmar wanaoungwa mkono na Israel ni watoto na wanawake Waislamu

 

Wakati huo huo afisa mmoja wa baraza la kijeshi la Myanmar mwaka 2015 alitembelea ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na kuonana na mkuu wa jeshi wa Israel.

Kwa mujibu wa takwimu za Umoja wa Mataifa, Waislamu 90 elfu wamekimbia makazi yao katika jimbo la Rakhine katika kipindi cha siku 10 zilizopita kutokana na ukatili mkubwa wanaofanyiwa na wanajeshi wa serikali ya Kibudha ya Myanmar.

Serikali ya nchi hiyo inawanyima Waislamu karibu milioni moja wa Rohingya hata haki zao za kimsingi kabisa kama vile uraia. 

Hadi hivi sasa maelfu ya Waislamu wa Rohingya wameshauawa na makumi ya maelfu  ya wengine wamelazimika kuyakimbia makazi yao.