India kuwafukuza wakimbizi Waislamu wa Myanmar wapatao 40,000
https://parstoday.ir/sw/news/world-i34465-india_kuwafukuza_wakimbizi_waislamu_wa_myanmar_wapatao_40_000
Serikali ya India imewasilisha ombi katika Mahakama ya Juu ya nchi hiyo la kutaka kutimuliwa makumi ya maelfu ya wakimbizi Waislamu wa kabila la Rohingya, waliokimbilia usalama wao nchini humo kutokana na kushadidi mashambulizi ya jeshi la Myanmar likishirikiana na Mabudha wenye misimamo mikali dhidi yao.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Sep 17, 2017 03:07 UTC
  • India kuwafukuza wakimbizi Waislamu wa Myanmar wapatao 40,000

Serikali ya India imewasilisha ombi katika Mahakama ya Juu ya nchi hiyo la kutaka kutimuliwa makumi ya maelfu ya wakimbizi Waislamu wa kabila la Rohingya, waliokimbilia usalama wao nchini humo kutokana na kushadidi mashambulizi ya jeshi la Myanmar likishirikiana na Mabudha wenye misimamo mikali dhidi yao.

Hatima ya wakimbizi hao wapatao 40 elfu wanaosemekana kuwasili nchini humo katika kipindi cha miaka 10 iliyopita itajulikana kesho Jumatatu.

Hoja ya serikali ya India ya kutaka kutimuliwa nchini humo wakimbizi hao raia wa Myanmar ni eti wanahatarisha usalama wa taifa.

Zeid Raad al-Hussein, Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa amekosoa vikali hatua ya serikali ya India ya kuwasilisha kesi mahakamani kutaka wakimbizi hao watimuliwe.

Wakimbizi Waislamu wa Rohingya waliokimbia Myanmar

Wakati huo huo, Ram Krishna Subedi, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nepal amenukuliwa na shirika la habari la AFP akisema kuwa, vyombo vya usalama nchini humo vimeimarisha usalama katika maeneo ya mipakani ili kuzuia wakimbizi wa Rohingya kuingia nchini humo.

Umoja wa Mataifa unasema kuwa zaidi ya Waislamu zaidi ya laki nne wa jamii ya Rohingya wamelazimishwa kukimbia miji na makazi yao tangu tarehe 25 mwezi uliopita wa Agosti, baada ya kuanza wimbi jipya la mashambulizi ya Mabudha wenye misimamo ya kuchupa mipaka wakishirikiana na jeshi la Myanmar dhidi yao.