-
Iran na Russia zaonya kuhusu kuhamishiwa magaidi wa Daesh Afghanistan
Dec 18, 2019 23:02Maafisa wa ngazi za juu wa usalama wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Russia wameonya kuhusu njama za makusudi za kuwahamishia wanachama wa kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh nchini Afghanistan.
-
Russia: Vikwazo haviwezi kuchukua nafasi ya udiplomasia
Dec 12, 2019 04:19Mwakilishi wa Russia katika Umoja wa Mataifa amesema haiwezekani kupatikana amani katika Rasi ya Korea kupitia njia ya vikwazo na mashinikizo na kwamba, vikwazo haviwezi kuchukua nafasi ya udiplomasia na njia ya utatuzi wa kisiasa.
-
Russia yafunga maelfu ya tovuti za Intaneti kwa sababu za ugaidi
Dec 11, 2019 22:48Serikali ya Russia imetangaza kuwa, tangu kuanza mwaka huu wa 2019 hadi hivi sasa imeshafunga mitandao 50 elfu ya Intaneti kutokana na kueneza taarifa za kigaidi nchini humo.
-
Mpango wa Pentagon wa kuongeza idadi ya askari wa Marekani barani Ulaya kwa kiwango ambacho hakijawahi kushuhudiwa
Dec 11, 2019 04:41Donald Trump, rais machachari na mwenye makeke wa Marekani amewahi kusikika mara kadhaa akiwalaumu na kuwakosoa waitifaki wa Washington wa barani Ulaya na hata kutishia kwamba, nchi yake haitakuwa tayari kuendelea kugharimika kwa ajili ya usalama wa nchi za bara hilo; hata hivyo mpango uliotangazwa na Wizara ya Ulinzi ya Marekani, Pentagon wa kuongeza idadi ya askari wa nchi hiyo barani Ulaya umeyatoa maanani madai hayo ya Trump.
-
Russia yafungiwa kushiriki michezo ikiwemo Olimpiki 2020 na kombe la dunia 2022
Dec 09, 2019 23:24Wakala wa Kimataifa wa Kupambana na Dawa za Kusisimua Misuli (WADA) limeifungia Russia kwa miaka minne kutoshiriki michuano mikubwa duniani ikiwemo michezo ya Olimpiki ya mwaka ujao wa 2020 itakayofanyika Tokyo Japan na Kombe la Soka la Duniani litakalofanyika nchini Qatar mwaka 2022.
-
Onyo kali la Russia juu ya kuharibika uhusiano wa nchi hiyo na Shirika la Kijeshi la NATO
Dec 09, 2019 23:23Katika miaka ya hivi karibuni uhusiano wa Russia na Muungano wa Kijeshi wa Nchi za Magharibi (NATO) hususan baada ya kuzuka mgogoro wa Ukraine mwaka 2014, umekuwa ni wa mzozo ambapo kiwango cha migogoro na makabiliano baina ya pande hizo mbili kimeendelea kukua mwaka baada ya mwaka.
-
Tahadhari ya Russia kuhusu uwezekano wa kusambaratika makubaliano ya nyuklia ya JCPOA
Dec 06, 2019 07:00Baada ya Marekani kujiondoa katika makubaliano ya nyuklia ya JCPOA mwezi Mei mwaka 2018 wanachama wengine wa makubaliano hayo wamekuwa wakitilia mkazo udharura wa kulindwa mapatano hayo ya kimataifa kutokana na umuhimu wake katika kulinda amani na usalama wa kimataifa.
-
Russia yapinga kuwa Iran pekee ndio itekeleze ahadi za JCPOA
Dec 01, 2019 08:36Kwa kuzingatia juhudi zinazofanywa na wanachama wa nchi za Magharibi katika mapatano ya nyuklia ya JCPOA za kutaka kutekeleza matakwa haramu ya Marekani ya kuitaka Iran kuwa ndio pekee iwe daima inafungamana na mapatano hayo ya nyuklia, serikali ya Russia imepinga wazi takwa hilo na kulitaja kuwa jambo lisilowezekana.
-
Sisitizo la Russia kuhusu haki ya Iran ya kupunguza uwajibikaji wake katika JCPOA
Nov 29, 2019 03:27Hatua ya Iran kupunguza utekelezaji wa ahadi zake katika mapatano ya nyuklia ya Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezwaji (JCPOA) imekabiliwa na ukosoaji mkali wa nchi za Ulaya katika kundi la 4+1 ambalo linazileta pamoja China, Russia, Ufaransa, Uingereza na Ujerumani. Ifahamike kuwa, Iran imechukua hatua hiyo baada ya Marekani kujiondoa katika mapatano ya JCPOA na nchi za Ulaya kushindwa kuchukua hatua za kivitendo za kufidia Marekani kujiondoa katika mapatano hayo ya kimataifa ya nyuklia.
-
Russia yakosoa hatua ya Marekani ya kutuma askari wengine nchini Saudia
Nov 20, 2019 21:34Serikali ya Russia kupitia Wizara ya Mambo ya Nje ya nchi hiyo imekosoa vikali hatua ya Marekani ya kutuma askari wengine nchini Saudi Arabia.