-
Rwanda yashambulia ndege ya kivita ya DRC kwa 'kukiuka' anga yake
Jan 25, 2023 11:52Serikali ya Kigali imesema imechukua 'hatua za kujilinda' baada ya ndege ya kijeshi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kukiuka anga ya Rwanda.
-
Rwanda yaituhumu DRC kuwa "imetengeneza" mauaji ya halaiki yanayodaiwa kufanywa na M23
Dec 22, 2022 07:35Rwanda imeishutumu serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwa "kutengeneza" mauaji, ambayo uchunguzi wa Umoja wa Mataifa ulisema yalifanywa na waasi wa M23 na kusababisha raia 131 kuuawa.
-
Rais Kagame aijia juu US kwa kutaka shujaa wa "Hotel Rwanda" aachiliwe
Dec 16, 2022 05:30Rais Paul Kagame wa Rwanda ameikosoa vikali Marekani kwa kuishinikiza serikali ya Kigali imuachie huru Paul Rusesabagina, nyota wa filamu ya "Hotel Rwanda" aliyegeuka na kuwa mkosoaji mkubwa wa serikali ya Kigali.
-
Wakimbizi wa DRC nchini Rwanda wakosoa kimya cha jamii ya kimataifa
Dec 13, 2022 07:16Maelfu ya wakimbizi raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo walioko nchini Rwanda wameikosoa jamii ya kimataifa kwa kufumbia macho mauaji yanayoendelea kufanywa na magenge ya waasi mashariki mwa DRC.
-
Rwanda yaafiki 'kusitishwa mapigano mara moja' mashariki mwa DR Kongo
Nov 19, 2022 07:12Rais wa zamani wa Kenya Uhuru Kenyatta na Rais Paul Kagame wa Rwanda wamekubaliana juu ya haja ya waasi wa M23 kusitisha mapigano na kuondoka katika maeneo waliyoyateka mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). Hayoa yameelezwa kwenye taarifa iliyotolewa na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).
-
Maelfu ya watu washiriki maandamano dhidi ya Rwanda mjini Goma Kongo DR
Nov 01, 2022 07:07Maelfu ya watu wameandamana katika mji wa Goma mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) dhidi Rwanda inayodaiwa kuwaunga mkono waasi wa M23, huku uhusiano baina ya nchi hizo mbili ukizidi kuharibika baada ya Kinshasa kumuita nyumbani kaimu balozi wake wa muda aliyeko Kigali.
-
Burundi yafungua mipaka yake na Rwanda baada ya miaka 5
Oct 24, 2022 04:02Serikali ya Burundi imetangaza kufungua mipaka ya ardhini ya nchi hiyo na jirani yake Rwanda, baada ya kufungwa kwa kipindi cha miaka mitano.
-
Kabuga, mtuhumiwa wa mauaji ya kimbari Rwanda akwepa ufunguzi wa kesi yake
Sep 29, 2022 12:21Felicien Kabuga anayetuhumiwa kushiriki katika mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 nchini Rwanda ameripotiwa kukataa kuhudhuria ufunguzi wa kesi dhidi yake katika Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ya mjini Hague nchini Uholanzi.
-
UN yawahamishia Rwanda watafuta hifadhi 100 kutoka Libya
Sep 02, 2022 12:06Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi UNHCR limetangaza kuwa limewahamishia nchini Rwanda makumi ya watu wanaotafuta hifadhi waliokuwa nchini Libya.
-
Mpango wa UK wawaacha bila makazi wahanga wa mauaji ya kimbari Rwanda
Sep 01, 2022 07:36Wahanga wa mauaji ya kimbari nchini Rwanda waliofurushwa katika mabweni walikokuwa wakiishi kutokana na mpango tata wa wakimbizi wa Uingereza, wanalalamika kuwa wameachwa bila pahala pa kuishi, licha ya mabweni hayo kusalia bila watu.