Rwanda yaituhumu DRC kuwa "imetengeneza" mauaji ya halaiki yanayodaiwa kufanywa na M23
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i91984-rwanda_yaituhumu_drc_kuwa_imetengeneza_mauaji_ya_halaiki_yanayodaiwa_kufanywa_na_m23
Rwanda imeishutumu serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwa "kutengeneza" mauaji, ambayo uchunguzi wa Umoja wa Mataifa ulisema yalifanywa na waasi wa M23 na kusababisha raia 131 kuuawa.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Dec 22, 2022 07:35 UTC
  • Rwanda yaituhumu DRC kuwa

Rwanda imeishutumu serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwa "kutengeneza" mauaji, ambayo uchunguzi wa Umoja wa Mataifa ulisema yalifanywa na waasi wa M23 na kusababisha raia 131 kuuawa.

Katika taarifa iliyotoa hapo jana, serikali ya Kigali imesema, 'mauaji ya halaiki ya Kishishe', uzushi wa serikali ya DRC ambayo iliyahusisha na M23, yameenea haraka bila kufanyiwa uchunguzi wowote wa kutafuta ukweli na chombo chochote kinachoaminika.
Taarifa hiyo ya serikali ya Rwanda imeendelea kueleza kwamba, kiuhakika tukio hilo lilikuwa makabiliano ya silaha kati ya M23 na makundi haramu yanayobeba silaha yenye mfungamano na jeshi la serikali ya Kongo DR.
Kundi la wanamgambo wa M23 nalo pia limekanusha kuhusika na mauaji ya raia zaidi ya 131 yanayodaiwa kufanywa mnamo Novemba 29 na 30 katika vijiji viwili vya Kishishe na Bambo jimboni Kivu Kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. 
Wanamgambo wa kundi la waasi la M23

Kinshasa inaituhumu jirani yake mdogo Rwanda kuwa inaliunga mkono kundi la waasi wa M23, madai ambayo yamekanushwa na Rwanda, lakini yanaungwa mkono na Marekani, Ufaransa, Ubelgiji na wataalamu wa Umoja wa Mataifa.

Wanamgambo hao wameteka eneo la mashariki mwa DRC lenye hali tete na lenye utajiri wa madini katika miezi ya hivi karibuni, na hivyo kuzusha mvutano kati ya serikali ya Kinshasa na Rwanda.../