-
Kuendelea mashambulizi dhidi ya Yemen na uwezekano mdogo wa kufanyika mazungumzo ya amani
Feb 05, 2016 03:41Huku mapigano katika maeneo tofauti ya Yemen yakipamba moto, Saudi Arabia imeendelea kukwamisha juhudi za kidiplomasia za kuutatua kisiasa mgogoro huo, suala ambalo limewafanya wanadiplomasia wa Umoja wa Mataifa kusema kuwa, ni jambo lililo mbali kufikiria kufanyika mazungumzo hayo katika siku za hivi karibuni.
-
Saudia yakosolewa kwa kuipa barabara jina la al-Baghdadi wa Daesh
Feb 03, 2016 04:09Wananchi wa Saudi Arabia hususan katika mitandao ya kijamii wamekosoa hatua ya ukoo wa Aal-Saud ya kuipa barabara moja mjini Riyadh jina la kiongozi wa kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh, Abu Bakr al-Baghdadi.
-
Zarif: Saudia haina budi kuacha sera zake za kiuhasama
Feb 02, 2016 23:49Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran ameitaka Saudi Arabia kuacha sera zake za kiuhasama dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu.
-
Saudia yakiri kukwama vitani Yemen
Feb 02, 2016 04:29Saudi Arabia imekiri kukwama katika vita vyake dhidi ya Yemen na kusema vita hivyo havina mshindi hata baada ya ndege zake za kivita kudondosha mabomu katika nchi hiyo masikini zaidi ya Kiarabu kwa muda wa takribani mwaka mmoja.
-
Wanajeshi na mamluki wa Saudi Arabia waendelea kuangamizwa nchini Yemen
Jan 31, 2016 23:25Wanajeshi zaidi ya 200 wa Saudia wameuawa na magari na zana za kijeshi za nchi hiyo kuharibiwa vibaya katika shambulio lililofanywa na jeshi la Yemen katika kituo cha anga cha al Anad kusini mwa Yemen.
-
Watu 5 wauawa katika hujuma msikitini Saudi Arabia
Jan 29, 2016 12:02Watu watano wameuawa kufuatia hujuma ya bomu na ufyatuaji risasi katika msikiti mmoja mjini al-Ahsa, katika mkoa wa Mashariki nchini Saudi Arabia.
-
HRW yakosoa ukiukaji wa haki za binadamu Saudia
Jan 29, 2016 04:49Shirika la Kutetea Haki za Binadamu la Human Rights Watch limekosoa ukiujaki wa haki za binadamu unaofanywa nchini Saudi Arabia. Shirika hilo limekosoa bikali utolewaji wa hukumu na adhabu kali dhidi ya wapinzani na vile vile kuendelea kushikiliwa kizuizini makumi ya wanaharakati wa haki za binadamu katika nchi hiyo ya Kiarabu.
-
Serikali ya Uingereza yazidi kukosolewa kwa kuiuzia Saudia silaha
Jan 27, 2016 23:44Matokeo ya utafiti uliofanywa na Umoja wa Mataifa kuhusiana na mashambulizi makubwa yanayofanywa na Saudi Arabia dhidi ya raia huko Yemen yamezidisha mashinikizo kwa serikali ya Uingereza kutokana na hatua yake ya kuiuzia silaha Riyadh.
-
UN: Mashambulizi ya Saudia yanalenga raia Yemen
Jan 27, 2016 05:32Kamati ya wataalamu ya Umoja wa Mataifa imesema kuwa Saudi Arabia na waitifaki wake wamekiuka haki za binadamu na sheria za kimataifa katika uvamizi na mashambulizi yao dhidi ya Yemen.