Saudia yakiri kukwama vitani Yemen
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i427-saudia_yakiri_kukwama_vitani_yemen
Saudi Arabia imekiri kukwama katika vita vyake dhidi ya Yemen na kusema vita hivyo havina mshindi hata baada ya ndege zake za kivita kudondosha mabomu katika nchi hiyo masikini zaidi ya Kiarabu kwa muda wa takribani mwaka mmoja.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 02, 2016 04:29 UTC
  • Saudia yakiri kukwama vitani Yemen

Saudi Arabia imekiri kukwama katika vita vyake dhidi ya Yemen na kusema vita hivyo havina mshindi hata baada ya ndege zake za kivita kudondosha mabomu katika nchi hiyo masikini zaidi ya Kiarabu kwa muda wa takribani mwaka mmoja.

Brigedia Jenerali Ahmed Asiri, msemaji wa jeshi la utawala wa Saudia amesema Jumatatu hii kuwa, ufalme huo umekwama katika vita visivyo na mshindi Yemen.

Amesema hivi sasa wataalamu wa kijeshi wa Marekani na Uingereza wanalisaidia jeshi la Saudia ili kuimarisha uwezo wake katika hujuma dhidi ya watu wa Yemen.

Yemen imekuwa ikishambuliwa na jeshi la Saudia na waitifaki wake tokea mwezi Machi mwaka jana kwa lengo la kumrejesha madarakani rais mtoro wa nchi hiyo Abdu Rabbu Mansur Hadi ambaye ni kibaraka wa utawala wa Riyadh.

Takwimu zainaonesha kuwa katika hujuma za kinyama za Saudia dhidi ya Yemen, watu karibu 8,270 wameuawa wengi wakiwa ni raia hasa watoto na wanawake. Idadi ya watoto Wayemeni waliouawa katika hujuma za Saudia ni 2,236. Aidha Saudia imedondosha mabomu katika mahospitali, misikiti, shule, viwanda, madaraja na miundombinu yote ya Yemen. Saudia pia inatumia mabomu yaliyopigwa marufuku katika hujuma zake za kuogofya Yemen.