Zarif: Saudia haina budi kuacha sera zake za kiuhasama
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i466-zarif_saudia_haina_budi_kuacha_sera_zake_za_kiuhasama
Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran ameitaka Saudi Arabia kuacha sera zake za kiuhasama dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 02, 2016 23:49 UTC
  • Zarif: Saudia haina budi kuacha sera zake za kiuhasama

Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran ameitaka Saudi Arabia kuacha sera zake za kiuhasama dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu.

Katika mkutano na waandishi wa habari pamoja na mwenzake wa Ujerumani, Frank-Walter Steinmeier hapa mjini Tehran, Muhammad Javad Zarif amesema utawala wa Aal-Saud umekuwa ukiendeleza sera za kiuhasama na kiuadui dhidi ya Iran na kwamba wakati umefika kwa utawala huo wa kifalme uangalie upya sera zake. Wakati huo huo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran kwa mara nyingine tena amelaani kitendo cha kikatili cha kumuua shahidi mwanazuoni wa Kiislamu nchini Saudia, Sheikh Nimr Baqir al-Nimr na kusema kuwa, mwanachuoni huyo hakufanya kosa lolote la kuhatarisha usalama wa Saudia. Mapema jana, Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Iran na Ujerumani walifanya mazungumzo kuhusu masuala ya kieneo na matukio ya kimataifa sambamba na kuimarisha uhusiano wa nchi mbili hizo. Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani leo Jumatano anatazamiwa kukutana na kufanya mazungumzo na Rais Hassan Rouhani pamoja na Ali Larijani, Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran yaani Bunge la Iran. Hii ni ziara ya pili kwa Steinmeir hapa nchini, tangu baada ya kusainiwa makubaliano ya nyuklia ya Iran yajulikanayo kama JCPOA, mwezi Julai mwaka jana.