Saudi Arabia yasisitiza kuondolewa haraka Yemen misaada ya kimataifa
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i1234-saudi_arabia_yasisitiza_kuondolewa_haraka_yemen_misaada_ya_kimataifa
Saudi Arabia imewataka wafanyakazi wa huduma za misaada ya kimataifa kuondoka haraka iwezekakavyo huko Yemen lengo likiwa ni kuzidisha mgogoro wa kibinadamu nchini humo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 14, 2016 09:53 UTC
  • Saudi Arabia yasisitiza kuondolewa haraka Yemen  misaada ya kimataifa

Saudi Arabia imewataka wafanyakazi wa huduma za misaada ya kimataifa kuondoka haraka iwezekakavyo huko Yemen lengo likiwa ni kuzidisha mgogoro wa kibinadamu nchini humo.

Jamie McGoldrick Mratibu wa Masuala ya Kibinadamu wa Umoja wa Mataifa huko Yemen amesema kuwa utawala wa Aal Saud umeutumia barua Umoja wa Mataifa ukitaka kusitishwa huduma za kibinadamu huko Yemen na kuwataka wafanyakazi wa kimataifa wa misaada ya kibinadamu kuondoka haraka iwezekanavyo nchini humo.

McGoldrick ameongeza kuwa Saudi Arabia imewasilisha ombi hilo huku ukubwa wa maafa ya kibinadamu yaliyosababishwa na mashambulizi ya Saudi ukizidi kuongezeka.

Mratibu wa Masuala ya Kibinadamu wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Yemen pia amezitaka pande zote zinazozozana huko Yemen kuheshimu sheria za kimataifa kuhusu haki za binadamu na kuruhusu misaada ya kibinadamu kuwafikia raia wa nchi hiyo.

Ripoti za Umoja wa Mataifa zinaeleza kuwa Wayemeni zaidi ya elfu nane wameuawa na wengine karibu ya elfu 28 wamejeruhiwa tangu kuanza mashambulizi ya Saudi Arabia huko Yemen mwezi Machi mwaka jana hadi sasa kwa uungaji mkono wa Marekani na baadhi ya nchi waitifaki wa Saudia. Watu milioni mbili na laki tano pia wamekuwa wakimbizi huko Yemen.