Pars Today
Wizara ya Ulinzi ya Saudi Arabia imethibitisha kuwa vikosi vya ulinzi vya Yemen vimefanya mashambulio makubwa ya makombora na ndege zisizo na rubani ndani ya ardhi ya nchi hiyo.
Waziri wa Afya wa Saudi Arabia ametangaza kuwa, kupata chanjo ya virusi vya corona ni sharti muhimu kwa watu wote wanaoazimia kutekeleza ibada ya Hija mwaka huu katika miji mitakatifu ya Makka na Madina.
Jeshi la Yemen limetangaza kutungua ndege ya kijasusi isiyo na rubani ya Saudi Arabia wakati ikiwa katika oparesheni ya kijasusi nchini humo.
Ripota Maalumu wa Umoja wa Mataifa Agnes Kalamar amesema ripoti ya serikali ya Marekani kuhusu mauaji ya mwandishi habari mkosoaji wa Saudia ni ya kuvunja moyo.
Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa ameeleza masikitiko yake kutokana na ukandamizaji unaofanywa na serikali ya Saudi Arabia dhidi ya raia wa nchi hiyo.
Dada wa mwanaharakati mmoja wa masuala ya kijamii wa Saudi Arabia ameushutumu vikali utawala wa ukoo wa Aal Saud kwa kuwatesa na kuwakandamiza wakosoaji wa utawala huo wa kiimla.
Mwakilishi wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Asarullah ya Yemen amesisitiza kuwa, Utawala wa Aal Saud unatumia viwanja vya ndege vya Saudia kutekeleza mashambulizi dhidi ya Yemen na kuyatahadharisha mashirika ya ndege kutotumia viwanja hivyo.
Msemaji wa harakati ya wananchi wa Yemen ya Ansarullah amesema kuwa mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa katika mgogoro wa Yemen, Martin Griffiths, ni Muingereza aliyevaa joho la Umoja wa Mataifa.
Mjumbe Malumu wa Umoja wa Mataifa katika Masuala ya Yemen amefanya mazungumzo na mshauri maalumu wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ambapo wamejadili matukio ya hivi karibuni ya Yemen.
Serikali ya Italia imesimamisha uuzaji wa silaha kwa Saudi Arabia na Umoja wa Falme za Kiarabu, baada ya wanaharakati na wabunge wa nchi hiyo ya Ulaya kuonya kuwa, silaha hizo zinatumika kukanyaga haki za binadamu nchini Yemen.