-
Wana wawili wa mfalme wa zamani wa Saudia waliotiwa mbaroni kwa ufisadi waachiliwa huru
Dec 30, 2017 04:11Baadhi ya duru zimetangaza habari ya kuachiliwa huru wana wawili wa mfalme wa zamani wa Saudi Arabia, Abdullah bin Abdul Aziz ambao walikuwa wametiwa nguvuni kwa tuhuma za ufisadi.
-
Watu wasiopungua 15 wauawa katika mashambulizi ya anga ya Saudi huko Sana'a na katika miji mingine
Dec 25, 2017 11:17Televisheni ya al Masirah imetangaza kuwa watu wasiopungua 15 wameuawa katika mashambulizi mapya ya anga ya Saudi Arabia katika maeneo mbalimbali huko Yemen, ukiwemo mji mkuu Sana'a.
-
Jeshi la Yemen: Tumeangamiza vifaru na magari ya deraya 1,200 ya wavamizi
Dec 24, 2017 23:16Wizara ya Ulinzi ya Yemen imesema kuwa, katika kipindi hiki cha karibu miaka mitatu ya uvamizi, jeshi la nchi hiyo na vikosi vya kujitolea vya wananchi vimefanikiwa kuteketeza zaidi ya vifaru na magari ya deraya 1,200 pamoja na kutungua ndege tano za kivita za muungano vamizi unaoongozwa na Saudi Arabia.
-
Sudan: Hatutaitambua mipaka mipya ya majini iliyowekwa na Misri na Saudia
Dec 21, 2017 12:47Sudan imewasilisha taarifa kwa Umoja wa Mataifa ikieleza kwamba endapo mipaka mipya ya majini iliyowekwa na Misri na Saudi Arabia itapitishwa rasmi haitoitambua katu mipaka hiyo.
-
Baada ya kushindwa njama zao dhidi ya Qatar na Yemen, kundi la Saudia lamalizia hasira zake kwa Uturuki
Dec 20, 2017 12:54Serikali ya Uturuki imekasirishwa sana na hatua ya waziri wa mambo ya nje wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) aliyetuma ujumbe kwenye ukurasa wake wa Twitter na kumtuhumu Rais Recep Tayyip Erdogan kuwa ni kutoka kizazi cha Waturuki waliofanya wizi mjini Madina na kukandamiza Waarabu wakati wa utawala wa Uthmaniyyah (Ottoman Empire).
-
Saudia yatangaza rasmi mpango wa kuanzisha uhusiano na utawala haramu wa Israel
Dec 16, 2017 22:06Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudi Arabia ametangaza rasmi kuwa utawala huo una mpango wa kuanzisha uhusiano kamili wa kidiplomasia na utawala haramu wa Israel huku Waislamu kote duniani wakiandamana dhidi ya utawala huo ambao unapanga kuufanya mji wa Quds kuwa mji wake mkuu.
-
Gazeti la Al Sharq lafichua: Saudi Arabia ni nchi iliyofisidika
Dec 16, 2017 04:37Nyaraka mpya zilizofichuliwa na gazeti la Al Sharq linalochapishwa nchini Qatar zinaonyesha kuwa uozo wa ufisadi umezagaa kwenye vyombo vya utawala nchini Saudi Arabia.
-
Msaidizi maalumu wa Spika: Madai ya Marekani dhidi ya Iran ni fedheha ya kisiasa
Dec 16, 2017 04:31Msaidizi maalumu wa Spika wa Bunge la Iran katika masuala ya kimataifa amesema madai yaliyotolewa na mwakilishi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa dhidi ya Iran ni fedheha ya kisiasa.
-
Jinai nyengine ya kinyama ya Saudia nchini Yemen; watu 115 wauawa na kujeruhiwa
Dec 14, 2017 12:19Utawala vamizi wa Aal Saud umeua watu wasiopungua 35 na kujeruhi wengine 80 baada ya kufyatua makombora saba yaliyolenga kambi na jela moja ya kijeshi katika mji mkuu wa Yemen, Sana'a.
-
Marekani yaionya Saudia dhidi ya mienendo yake Mashariki ya Kati
Dec 09, 2017 03:53Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Marekani ameitahadharisha Saudi Arabia juu ya matokeo mabaya ya vitendo vyake katika eneo la Mashariki ya Kati.