Gazeti la Al Sharq lafichua: Saudi Arabia ni nchi iliyofisidika
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i37671-gazeti_la_al_sharq_lafichua_saudi_arabia_ni_nchi_iliyofisidika
Nyaraka mpya zilizofichuliwa na gazeti la Al Sharq linalochapishwa nchini Qatar zinaonyesha kuwa uozo wa ufisadi umezagaa kwenye vyombo vya utawala nchini Saudi Arabia.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Dec 16, 2017 04:37 UTC
  • Gazeti la Al Sharq lafichua: Saudi Arabia ni nchi iliyofisidika

Nyaraka mpya zilizofichuliwa na gazeti la Al Sharq linalochapishwa nchini Qatar zinaonyesha kuwa uozo wa ufisadi umezagaa kwenye vyombo vya utawala nchini Saudi Arabia.

Nyaraka zilizotolewa na gazeti hilo zinaonyesha kuwa ufisadi mkubwa wa kisiasa umeenea ndani ya taasisi za utawala wa Aal Saud ambazo zimeyageuza maslahi ya Saudi Arabia kuwa maslahi yao binafsi huku raia wa kawaida wakikosa hata haki na huduma za msingi ambazo kila serikali duniani huwapatia raia wake. 

Nyaraka hizo zilizotolewa kwenye tovuti ya gazeti hilo zinaonyesha jinsi utawala wa Aal Saud unavyofunika uozo wa ufisadi unaofanywa na wanawafalme wengi wa Saudia kiasi cha kuweza kuthubutu kueleza kwamba: kampeni ya kupambana na ufisadi iliyoanzishwa hivi karibuni na mrithi wa ufalme wa nchi hiyo Muhammad bin Salman si ya kupambana na ufisadi ila ni ya uchu na tamaa aliyonayo bin Salman kwa utajiri wa Saudi Arabia.

Baadhi ya viongozi, wanawafalme na shakshia waliotiwa nguvuni katika 'kampeni ya kupambana na ufisadi'

Kwa mujibu wa ripoti ya gazeti la Al Sharq, balozi za Saudia nje ya nchi badala ya kufanya kazi ya kuimarisha uhusiano na kulinda maslahi ya nchi na raia wa Saudi Arabia wanaoishi kwenye nchi nyenginezo, zimegeuzwa kuwa ofisi za utoaji huduma za binafsi kwa watu wenye satua, ukoo wa kifalme unaotawala nchi hiyo pamoja na watu wao wa karibu.../