Ndege za kivita za Saudia zaua wanawake 10 magharibi mwa Yemen
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i38303-ndege_za_kivita_za_saudia_zaua_wanawake_10_magharibi_mwa_yemen
Ndege za kivita za Saudi Arabia zimeshambulia shamba moja magharibi mwa Yemen na kuua wanawke wasiopungua 10 waliokuwa katika eneo hilo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Dec 30, 2017 10:50 UTC
  • Ndege za kivita za Saudia zaua wanawake 10 magharibi mwa Yemen

Ndege za kivita za Saudi Arabia zimeshambulia shamba moja magharibi mwa Yemen na kuua wanawke wasiopungua 10 waliokuwa katika eneo hilo.

Kwa mujibu wa ripoti ya Jumamosi ya televisheni ya Al-Masirah, ndege za kivita za Saudia zimedondosha mabomu katika shamba lililo katika Wilaya ya Khoukha mkoani al-Hudaydah katika ukanda wa pwani wa magharibi mwa nchi hiyo.

Hakuna maelezo zaidi yaliyotolewa kuhusu jinai hiyo mpya ya Saudia dhidi ya watu wa Yemen.

Tangu mwezi Machi mwaka 2015, Saudia, ikisaidiwa na kuungwa mkono na baadhi ya nchi za Kiarabu na Marekani ilianzisha mashambulio ya kinyama dhidi ya Yemen kwa lengo la kutaka kumrejesha madarakani kibaraka wake Abd Rabbuh Mansur Hadi, rais wa nchi hiyo aliyejiuzulu na kuitoroka nchi.

Watoto wanaougua kipindupindu Yemen

Hadi sasa watu zaidi ya 13,000, wengi wao wakiwa watoto na wanawake, wameuawa na mamilioni ya wengine kuwa wakimbizi kutokana na mashambulizi yanayoendelea kufanywa na Saudi Arabia na washirika wake dhidi ya nchi hiyo.

Aidha Shirika la Afya Duniani (WHO) limetangaza kuwa wahanga wa ugonjwa wa kipindupindu Yemen wamefikia 2, 200 tokea mwezi Aprili. Aidha Ripoti ya WHO imebainisha kuwa, hadi sasa watu milioni moja wanaugua kipindupindu katika maeneo mbalimbali ya Yemen. Saudi Arabia inatuhumiwa kueneza kwa makusudi ugonjwa wa kipindupindu Yemen kama sehemu ya vita vya kibiolojia dhidi ya nchi hiyo.