-
Wahalifu wanaotafuta damu ya watoto 1000 kufanya kafara Gabon wamekuwa janga + Sauti
Jan 28, 2020 02:30Wazazi katika mji mkuu wa Gabon, Libreville, Jumatatu, Januari 27, 2020 hawakuwaruhusu watoto wao kwenda skuli licha ya serikali kuweka ulinzi mkali katika skuli zote za mji huo mkuu. Wazazi hao wanasema kuwa hatua hiyo pekee haiwezi kuwazuia wahalifu wanaotafuta damu za watoto elfu moja kama kafara ya kuwabakisha madarakani. Mossi Mwasi na maelezo zaidi kutoka Brazzaville.
-
Chama cha FDC chailaumu vikali serikali ya Uganda + Sauti
Jan 20, 2020 16:18Kwa mara nyingine tena, mwanasiasa mkongwe katika chama cha FDC nchini Uganda, Daktari Kizza Besigye ameikosoa vikali serikali ya Rais Yoweri Museveni kutokana na ubabe na ukandamizaji unaofanywa na vyombo vya dola dhidi ya wapinzani. Kigozi Ismail na maelezo zaidi kutoka Kampala.
-
Wakazi wa kaskazini mwa Bujumbura waendelea kuteseka kwa madhara ya mafuriko + Sauti
Jan 07, 2020 08:31Waathiriwa wa mafuriko katika baadhi ya maeneo ya kaskazini mwa Bujumbura waliopiga kambi katika madarasa ya shule wametakiwa kuondoka ili kuruhusu sehemu ya pili ya mwaka wa shule kuanza. Hata hivyo raia hao wanalalamika kutokuwa na sehemu ya kwenda. Hali hiyo imepelekea baadhi ya shule katika eneo hilo kuakhirisha kufungua muhula mpya wa masomo. Hamida Issa na maelezo zaidi kutoka Bujumbura…
-
Waislamu Zanzibar wahimizwa kujifunza elimu ya ndoa ili kuepuka talaka holela + Sauti
Dec 27, 2019 15:50Waislamu visiwani Zanzibar hasa vijana wametakiwa kulipa umuhimu suala la elimu ya ndoa ili kupunguza wimbi la talaka za kiholela ambazo kimsingi zinahesabiwa ni sehemu moja ya kukanyaga haki za watoto. Hayo na mengineyo yamo kwenye ripoti ya kila wiki ya matukio ya Kiislamu, Afrika Mashariki, kama inavyoletwa kwenu na mwandishi wetu wa Zanzibar, Harith Subeit.
-
Hali ya utulivu yarejea Bangui, Jamhuri ya Afrika ya Kati baada ya mapigano + Sauti
Dec 27, 2019 15:48Hali ya utulivu imerejea katika mji mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Bangui baada ya siku mbili za mapigano baina ya makundi mawili hasimu. Mapigano hayo yamesababisha zaidi ya watu 30 kuuawa na wengine wengi kujeruhiwa. Mossi Mwasi na maelezo zaidi…
-
Uganda yapongezwa na WHO kwa kukazania afya ya jamii + Sauti
Dec 27, 2019 15:45Serikali ya Uganda imepongezwa kwa kusimamia na kukazania vyema afya katika jamii kuanzia mashinani. Pongezi hizo zimetolewa na Shirika la Afya Duniani, WHO. Kigozi Ismail na maelezo zaidi kutoka Kampala…
-
Waziri wa zamani wa DRC ataka Rwanda ivamiwe na kugeuzwa mkoa ili mashariki mwa DRC kuwe salama + Sauti
Dec 25, 2019 10:44Waziri Mkuu wa zamani wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Adolphe Muzito amesema kuwa, njia pekee ya kumaliza uasi mashariki mwa nchi hiyo ni kuivamia nchi jirani ya Rwanda na kuigeuza kuwa mkoa wa DRC. Mossi Mwasi na maelezo zaidi.
-
Mashinikizo ya wananchi yailazimisha serikali DRC kufuta sherehe za kukabidhiwa madaraka Tshisekedi + Sauti
Dec 23, 2019 09:59Serikali ya jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imelazimika kufutilia mbali sherehe za kupokezana madaraka kwa njia ya amani baina ya rais mstaafu wa nchi hiyo Joseph Kabila na rais wa hivi sasa Felix Tshisekedi. Hii in baada ya wananchi na asasi za kiraia kulalamikia gharama kubwa za hafla hizo zilizotazamiwa kufanyika tarehe 24 Januari mwakani. Mwandishi wetu Mossi mwazi na maelezo zaidi.
-
Mkuu wa Mkoa wa Tabora afuta mapumziko ya Mwaka Mpya; watu wakalime pamba + Sauti
Dec 15, 2019 16:20Nchini Tanzania, Mkuu wa mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri, ameagiza kuakhirishwa likizo ya A-Mass na mwaka mpya kwa maafisa wa kilimo na maafisa wote katika kipindi hiki cha mvua, ili watoke waende vijijini wakawahimize wananchi kulima pamba kwa ubora unaotakiwa. Ammar Dachi na maelezo zaidi kutoka Dar es Salaam, Tanzania
-
ACT-Wazalendo yalalamika kufanyiwa hujuma visiwani Zanzibar + Sauti
Dec 02, 2019 17:01Viongozi wa chama cha ACT Wazalendo visiwani Zanzibar wametahadharisha kuhusu madhara yanayoweza kutokea kutokana na kile wanachoamini ni hujuma za makusudi zinazoendeshwa dhidi ya viongozi wa chama hicho visiwani Unguja na Pemba. Harith Subeit na maelezo zaidi kutoka Zanzibar.