-
Tume ya Uchaguzi Uganda yakumbwa na kashfa nyingine mpya + Sauti
Dec 02, 2019 16:59Baada ya Tume ya Uchaguzi nchini Uganda kufunguliwa mashtaka ya makosa ya kukaa ofisini kinyume cha sheria, tume hiyo sasa imekumbwa na kashfa nyingine ya kisiasa... Kigozi Ismail na maelezo zaidi kutoka Kampala.
-
Viongozi wa Kenya wazindua ripoti ya BBI + Sauti
Nov 28, 2019 07:02Viongozi nchini Kenya wamezindua ripoti ya uwiano na utangamano wa kisiasa huku wakifanya juhudi za kuleta muamko mpya wa kisiasa na mshikamano katika kila fani ya maisha nchini humo. Seifullah Murtadha na maelezo zaidi kutoka Mombasa...
-
Waziri wa Mambo ya Ndani wa Burundi atembelea eneo aliloshambuliwa na waasi + Sauti
Nov 25, 2019 16:04Wiki moja baada ya kushambuliwa na watu wenye silaha walotajwa na jeshi la Burundi kwamba walitokea katika nchi jirani ya Rwanda, Waziri wa Mambo ya Ndani wa Burundi, Pascal Barandagiye, ametembelea tarafa ya Mabayi na kuwataka raia na watawala kuwa makini juu ya suala la usalama wakati huu ambapo imebakia miezi 6 tu kabla ya kufanyika uchaguzi nchini Burundi. Hamida Issa na maelezo zaidi kutoka Bujumbura.
-
Zaidi ya familia 50 zahamishwa katika mpaka wa Uganda na Kenya kutokana na mafuriko + Sauti
Nov 25, 2019 15:40Familia zaidi ya 50 zimehamishwa kutoka kwenye mpaka wa Uganda na Kenya kutokana na kuhofia maafa yanayoweza kusababishwa na mvua kubwa zinazonyesha mfululizo. Kigozi Ismail na ripoti zaidi kutoka Kampala.
-
Idadi ya waliofariki dunia kwenye ajali ya ndege DRC yaongezeka + Sauti
Nov 25, 2019 15:36Idadi ya watu waliofariki dunia baada ya kuanguka ndege ndogo ya abiria katika mji wa Goma wa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imeongezeka na kufikia watu 29 wakiwemo watu tisa wa familia moja. Watu wengine 19 wamejeruhiwa. Ndege hiyo iliyokuwa inaelekea Beni kutokea Goma ilianguka juu ya nyumba ya watu na kuua watu waliokuwemo ndani ya nyumba hiyo. Mossi Mwassi na maelezo zaidi
-
Matukio ya Kiislamu: Kitabu kipya cha Maulidi kuzinduliwa Zanzibar, kitagaiwa bure + Sauti
Nov 01, 2019 16:31Kitabu kipya kinachozungumzia mazazi ya Bwana Mtume Muhammad SAW kuzinduliwa visiwani Zanzibar sambamba na kuingia mwezi wa Mfunguo Sita ambapo hushamiri sana sherehe za Maulidi ya mtukufu huyo wa daraja. Hayo na mengineyo yamo kwenye ripoti ya kila wiki ya matukio ya Kiislamu iliyoandaliwa na mwandishi wetu wa Zanzibar, Harith Subeit…
-
Bunge la Uganda lataka kuondolewa nyongeza ya karo Chuo Kikuu Makerere + Sauti
Nov 01, 2019 16:28Bunge la Uganda limependekeza kuondolewa nyongeza ya karo baada ya kuongezeka maandamano na upinzani mkubwa wa wanachuo wa Chuo Kikuu cha Makerere. Maelezo zaidi na mwandishi wetu wa Kampala, Kigozi Ismail.
-
Mvua kubwa zazidi kusababisha maafa katika nchi mbalimbali za Afrika + Sauti
Oct 30, 2019 16:41Mvua kubwa zinazonyesha katika nchi za Afrika ya Kati hususan Cameroon na Jamhuri ya Afrika ya Kati zimesababisha maafa makubwa ya watu wengi kupoteza maisha yao na pia makazi. Kwa maelezo zaidi, tumtegee sikio mwandishi wetu wa Afrika ya Kati. Mosi Mwasi, akiripoti kutoka Brazzaville
-
Kumbukumbu ya siku aliyofariki dunia Bwana Mtume Muhammad SAW + Sauti
Oct 28, 2019 05:17Katika kumbukumbu ya kifo cha Bwana Mtume Muhammad SAW nchini Tanzania, viongozi wa dini ya Kiislamu wametakiwa kuweka mikakati imara ya kuwalingania vijana na sio kuwaona ni waasi waliopotoka. Amari Dachi na taarifa zaidi akiripoti kutoka Dar es Salaam.
-
Kenya yaomba msaada wa UN kupambana na majangili + Sauti
Oct 24, 2019 07:37Kenya imesalimu amri na kuuomba Umoja wa Mataifa uisaidie kukabiliana na biashara za uwindaji haramu. Serikali ya Kenya imesema, licha ya juhudi zake za kupambana na ujangili, lakini bado kazi ni pevu na inahitajia msaada wa kimataifa. Mwandishi wetu Seifullah Murtadha na maelezo zaidi kutoka Mombasa, Kenya.