Idadi ya waliofariki dunia kwenye ajali ya ndege DRC yaongezeka + Sauti
Nov 25, 2019 12:06 UTC
Idadi ya watu waliofariki dunia baada ya kuanguka ndege ndogo ya abiria katika mji wa Goma wa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imeongezeka na kufikia watu 29 wakiwemo watu tisa wa familia moja. Watu wengine 19 wamejeruhiwa. Ndege hiyo iliyokuwa inaelekea Beni kutokea Goma ilianguka juu ya nyumba ya watu na kuua watu waliokuwemo ndani ya nyumba hiyo. Mossi Mwassi na maelezo zaidi
Tags