-
Sayyid Hassan Nasrullah: Jihadi ya Ujenzi ni sehemu ya muqawama
Jul 27, 2019 07:17Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Lebanon Hizbullah amesema kuwa Jihad ya Ujenzi ni moja ya taasisi kongwe zaidi nchini Lebanon ambayo mbali na kutoa huduma za kiuchumi kwa wananchi wa Lebanon, jihadi hiyo inajishughulisha na kuondoa masalia ya mashambulio ya utawala wa Kizayuni nchini humo.
-
Sayyid Nasrullah: Muqawama upo katika kiwango bora kabisa
Jul 20, 2019 02:37Sayyid Hassan Nasrullah, Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon amesema kuwa, mapambano na muqawama upo katika kiwango cha juu kabisa na kusisitiza kwamba, siasa za chukki na uadui za Marekani na utawala haramu wa Israel katika eneo la Asia Magharibi zitashindwa na kugonga mwamba.
-
Mahojiano ya Sayyid Hassan Nasrullah katika kumbukumbu ya kutimia mwaka 13 tangu baada ya vita vya siku 33
Jul 13, 2019 13:31Sayyid Hassan Nasrullah Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon jana usiku alifanya mahojiano na televisheni ya al Manar kwa mnasaba wa kumbukumbu ya mwaka wa 13 tangu baada ya vita vya siku 33 huko Lebanon na kubainisha taathira za vita hivyo kwa Lebanon na eneo zima la Mashariki ya Kati.
-
Sayyid Hassan Nasrullah atuma ujumbe kwa mnasaba wa Siku ya Kimataifa ya Quds
May 30, 2019 04:13Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon ametuma ujumbe kwa njia ya video na kuashiria umuhimu wa Siku ya Kimataifa ya Quds. Nasrullah amewatolea wito walimwengu kushiriki kwa wingi katika maandamano ya siku hiyo.
-
Nasrallah: Wote wanawajibika kukabiliana na mpango wa 'Muamala wa Karne"
May 26, 2019 06:27Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesema: "Wote wanawajibika kukabiliana na mpango wa Marekani wa "Muamala wa Karne" ambao lengo lake ni kusambaratisha kadhia ya Palestina.
-
Hizbullah: Israel itaangamia ikithubutu kuishambulia Lebanon
May 03, 2019 07:45Katibu Mkuu wa Harakati ya Muqawama ya Hizbullah ya Lebanon ameutahadharisha utawala wa Tel Aviv dhidi ya kuanzisha vita vipya dhidi ya Lebanon na kusisitiza kuwa, wanajeshi wa utawala haramu wa Israel watasambaratishwa na kuangamizwa iwapo vita hivyo vitaibuka.
-
Sayyid Hassan Nasrullah: Daesh (ISIS) ni zao la Saudia na fikra ya Uwahabi
Apr 22, 2019 17:25Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon Sayyid Hassan Nasrullah amesema kuwa, kundi la kigaidi na ukufurishaji la Daesh (ISIS) ni zao la Saudi Arabia na fikra za Uwahabi na amesisitiza kwamba makundi mengi ya kigaidi yanapata mikopo ya fedha kutoka taasisi mbalimbali za kidini nchini Saudia na kutumia fikra hizo hizo za Uwahabi kufanya mauaji na jinai dhidi ya mataifa ya Waislamu.
-
Nasrullah: Hatua ya US dhidi ya IRGC ni thibitisho kuwa Washington imefeli katika eneo
Apr 11, 2019 13:56Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Lebanon (Hizbullah) sambamba na kulaani hatua ya Rais Donald Trump ya kuliweka Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu IRGC katika orodha ya Marekani ya makundi ya kigaidi amesisitiza kuwa, kitendo hicho ni ithibati tosha kuwa Washington imefeli katika njama zake ghalati katika eneo la Asia Magharibi.
-
Nasrullah: Hatua ya Trump ya kuitambua miinuko ya Golan kuwa mali ya Israel ni kuutusi Ulimwengu wa Kiislamu
Mar 27, 2019 08:06Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon amesema kuwa, hatua ya Rais Donald Trump wa Marekani ya kuitambua rasmi miinuko ya Golan kuwa ni mali na miliki ya utawala haramu wa Israel ni kuzitusi na kuzivunjia heshima nchi za Ulimwengu wa Kiislamu na Kiarabu.
-
Sayyid Hassan Nasrullah: Uimara wa muqawama umesambaratisha njama zote za Marekani
Mar 09, 2019 04:46Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon Sayyid Hassan Nasrullah amesema kuwa, Marekani ilikuwa na njama kubwa tofauti kwa ajili ya kuhitimisha muqawama mwaka 2006, lakini uimara wa muqawama ukafanikisha kusambaratisha njama zote hizo.