Sayyid Hassan Nasrullah: Jihadi ya Ujenzi ni sehemu ya muqawama
Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Lebanon Hizbullah amesema kuwa Jihad ya Ujenzi ni moja ya taasisi kongwe zaidi nchini Lebanon ambayo mbali na kutoa huduma za kiuchumi kwa wananchi wa Lebanon, jihadi hiyo inajishughulisha na kuondoa masalia ya mashambulio ya utawala wa Kizayuni nchini humo.
Akizungumza jana katika eneo la Dhahiya kusini mwa Beirut kwa mnasaba wa maadhimisho ya kutimia mwaka wa 31 tangu kuasisiwa Taasisi ya Jihadi ya Ujenzi huko Lebanon, Sayyid Hassan Nasrullah Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ameeleza kuwa Taasisi ya Jihadi ya Ujenzi ni sehemu ya siasa endelevu za kimuqawama pamoja na mapambano ya silaha na kisiasa.
Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon ameashiria pia vikwazo vya Marekani dhidi ya Taasisi hiyo ya Jihadi Sazandegi ya nchi hiyo na kueleza kuwa: Utawala wa Kizayuni ulifanya kila uwezalo ili kuwaonyesha wananchi wa Lebanon uharibifu uliosababishwa katika vita vya siku 33 mwaka 2006 kuwa ni pigo na ishara ya kushindwa kwao hata hivyo muda mfupi baada ya Israel kusimamisha vita Taasisi ya Jihadi ya Ujenzi ilianza mara moja kuzikarabati nyumba na kukamilisha kazi hiyo katika muda wa miaka mitano.