Sayyid Nasrullah: Muqawama upo katika kiwango bora kabisa
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i54871-sayyid_nasrullah_muqawama_upo_katika_kiwango_bora_kabisa
Sayyid Hassan Nasrullah, Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon amesema kuwa, mapambano na muqawama upo katika kiwango cha juu kabisa na kusisitiza kwamba, siasa za chukki na uadui za Marekani na utawala haramu wa Israel katika eneo la Asia Magharibi zitashindwa na kugonga mwamba.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Jul 20, 2019 02:37 UTC
  • Sayyid Nasrullah: Muqawama upo katika kiwango bora kabisa

Sayyid Hassan Nasrullah, Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon amesema kuwa, mapambano na muqawama upo katika kiwango cha juu kabisa na kusisitiza kwamba, siasa za chukki na uadui za Marekani na utawala haramu wa Israel katika eneo la Asia Magharibi zitashindwa na kugonga mwamba.

Sayyid Nasrullah amesema hayo kkatika mazungumzo yake na Hossein Amir-Abdollahian, msaidizi maalumu wa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika masuala ya kimataifa ambapo sambamba na kuthamini uungaji mkono wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, serikali na taifa la Iran katika kusaidia kuleta amaani na usalama wa eneo amesema kuwa, kama alivyosema Ayatullah Sayyid Ali Khamenei ni kuwa, Marekani haina ubavu wa kuitwisha Iran vita.

Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon ameongeza kuwa, serikali ya Marekani inatambua vyema kwamba, kama kutatokea vita dhidi ya Iran, eneo lote la Mashariki ya Kati litashughulishwa na vita hivyo na bila shaka mwenye kuhitimisha vita hivyo haitakuwa Washington.

Rais Donald Trump wa Marekani

Nasrullah ameeleza kuwa, mpango wa kisiasa na kidemokrasia wa Iran wa kufanyika kura ya maoni miongoni mwa wakazi asili na wa kihistoria wa Palestina kwa kuhudhuria wafuasi wa dini zote za mbinguni mbali na Mayahudi na Wakristo ni mpango wa kimantiki na unaoangalia mambo kwa uhalisia wake.

Aidha Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon amesema kuwa, mpango wa Marekani-Israel wa 'Muamala wa Karne" hauna maana na hautafanikiwa kufikia malengo yake.