-
Wagombea 15 wa urais Senegal wataka uchaguzi ufanyike kabla ya muhula wa Rais Sall kumalizika
Feb 20, 2024 07:05Wagombea 15 kati ya 20 walioidhinishwa kugombea katika uchaguzi wa urais wa Senegal ambao uliakhirishwa kufanyika mwezi huu wa Februari wametaka uchaguzi huo mpya uwe umeshafanyika kabla ya tarehe Pili Aprili.
-
Baraza la Katiba Senegal: Uamuzi wa Bunge wa kuidhinisha kuakhirishwa uchaguzi ni "kinyume na Katiba"
Feb 16, 2024 07:51Baraza la Katiba la Senegal limetoa hukumu na kutangaza kwamba uamuzi uliopitishwa na bunge wa kuakhirisha uchaguzi wa rais wa Februari 25 hadi Disemba haukuendana na Katiba.
-
Maandamano ya wapinzani Senegal yaahirishwa baada ya kupigwa marufuku na serikali
Feb 13, 2024 12:01Maandamano yaliyokuwa yamepangwa kufanyika leo huko Senegal kupinga hatua ya Rais Macky Sall wa nchi hiyo ya kuakhirisha uchaguzi wa rais, yameakhirishwa baada ya serikali kuyapiga marufuku.
-
AU: Tuna wasiwasi kuhusu kuakhirishwa uchaguzi wa Rais Senegal
Feb 05, 2024 15:32Umoja wa Afrika (AU) umesema kuwa unatiwa wasiwasi na hatua ya Senegal ya kuakhirisha uchaguzi wa rais wa nchi hiyo.
-
Polisi wapambana na waandamanaji Senegal wanaolalamikia kuakhirishwa uchaguzi wa rais
Feb 05, 2024 06:46Wafuasi wa vyama vya upinzani na polisi wamepambana katika mji mkuu wa Senegal Dakar baada ya Rais Macky Sall kutangaza kuakhirisha kwa muda usiojulikana uchaguzi wa rais uliopangwa kufanyika Februari 25, na hivyo kuzusha wasiwasi kimataifa.
-
Rais wa Senegal aakhirisha uchaguzi wa rais wa Februari 25 kwa muda usiojulikana
Feb 04, 2024 03:22Rais Macky Sall wa Senegal ametangaza kuakhirisha kwa muda usiojulikana uchaguzi wa urais uliopangwa kufanyika Februari 25, saa chache kabla ya kampeni rasmi kuanza.
-
Chama cha upinzani chataka kuakhirishwa uchaguzi wa rais Senegal
Feb 03, 2024 07:29Chama cha Democratic cha Senegal (PDS) kimewasilisha muswada Bungeni unaotaka kuakirishwa uchaguzi wa rais ulioratibiwa kufanyika baadaye mwezi huu.
-
Kiongozi wa upinzani Senegal aondolewa katika orodha ya wagombea urais
Jan 21, 2024 07:50Baraza la Katiba la Senegal Jumamosi lilichapisha orodha ya mwisho ya wagombea 20 wa uchaguzi wa rais uliopangwa kufanyika nchini humo Februari 25 ambayo haiwajumuishi kiongozi wa upinzani aliyefungwa Ousmane Sonko, na Karim Wade, mtoto wa rais wa zamani wa Rais wa nchi hiyo Abdoulaye Wade.
-
Ousmane Sonko apatikana na hatia, hataruhusiwa kugombea urais Senegal
Jan 05, 2024 07:44Mahakama ya Juu ya Senegal imethibitisha hukumu iliyotolewa Mei mwaka jana na Mahakama ya Rufaa ya kifungo cha miezi sita jela dhidi ya kinara wa upinzani nchini humo, Ousmane Sonko, kwa kumkashifu Waziri wa Utalii, Mame Mbaye Niang.
-
Mahakama Senegal 'yaridhia' kiongozi wa upinzani agombee urais
Dec 15, 2023 10:32Mahakama Kuu mjini Dakar imeamuru kusajiliwa upya kwa Ousmane Sonko, kiongozi wa upinzani nchini Senegal katika daftari la wapigakura, na hivyo kumruhusu kuwa mgombea urais.