Pars Today
Vita kati ya majenerali hasimu huko Sudan jana Alhamisi viliingia katika mwezi wake wa tatu na haijulikani lini vitamalizika. Ndege za kivita za jeshi la Sudan jana Alkhamisi zilifanya mashambulizi kwa mara ya kwanza katika mji wa kusini mwa nchi hiyo wa El- Obeid' na kuvituhumu Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) kuwa ndivyo vilivyomteka nyara na kumuuwa Gavana wa Darfur.
Vikosi vya Msaada wa Haraka vya Sudan (RSF) vimewateka nyara askari wa jeshi la nchi hiyo katika jimbo la Darfur Kusini.
Jumuiya ya Maendeleo ya Kiserikali (IGAD) inafanya mkutano wa kilele nchini Djibouti leo Jumatatu ili kuzishawishi pande mbili katika mgogoro wa Sudan kufanya mazungumzo ya kumaliza mapigano ya wenyewe kwa wenyewe, wakati huu ambapo mji mkuu Khartoum unashuhudia mapigano makali.
Mgogoro wa kisiasa na vita vya kuwania madaraka vinaendelea kutokota nchini Sudan licha ya jitihada zote za kimataifa na kikanda zinazofanyika kwa ajili ya kurejesha amani nchini huko. Katika hatua ya karibuni, Wizara ya Mambo ya Nje ya Sudan imemfukuza Volker Perthes aliyekuwa Mjumbe wa Umoja wa Mataifa na kumtaja kuwa mtu asiyetakikana nchini humo.
Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa Unicef limeeleza kuwa, watoto wasiopungua 300 wa rika mbalimbali wakiwemo wachanga wameokolewa kutoka katika kituo cha kulelea mayatima huko Khartoum mji mkuu wa Sudan baada ya kutelekezwa huko huku mapigano yakiendelea nchini humo.
Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imesema raia kumi wa nchi hiyo wameuawa katika mashambulizi ya Jeshi la Sudan ndani ya Chuo Kikuu kimoja mjini Khartoum, huku mapigano yakishtadi nchini Sudan kati ya jeshi na wapiganaji wa Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF).
Msemaji wa jeshi la Sudan jana alieleza kuwa jeshi hilo limesitisha kushiriki katika mazungumzo na Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) ambavyo limekuwa likipigana navyo kwa wiki kadhaa sasa kwa ajili ya kuidhibiti Sudan.
Umoja wa Afrika umesisitiza kuwa, unapinga uingiliaji wa kigeni katika masuala ya Sudan na kwamba, hilo ni jambo lisilokubalika.
Mashirika mawili ya Umoja wa Mataifa yameonya kuwa, mamilioni ya watu wapo katika hatari ya kufa njaa katika nchi za Sudan, Haiti, Burkina Faso, na Mali.
Mkuu wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AU) amesiistiza ulazima wa kusimamishwa vita haraka iwezekanavyo kati ya pande zinazopigana nchini Sudan.