Pars Today
Makundi ya Muungano wa Uhuru na Mabadiliko Sudan yametoa wito wa kuitaka Jamii ya Kimataifa ichukue hatua kuzuia kutokea vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo.
Jenerali Mkuu wa Sudan jana alieleza kuwa jeshi la nchi hiyo lingali lina nia ya kukabidhi madaraka kwa serikali ya kiraia. Hayo ni matamshi ya kwanza kutolewa kiongozi wa baraza la uongozi wa kijeshi la Sudan Jenerali Abdel Fattah al Burhan tangu kuanza karibu wiki moja iliyopita mapigano makali huko Sudan kati ya vikosi vitiifu kwa kiongozi huyo wa jeshi na askari kikosi cha radiamali ya haraka (RSF).
Msemaji wa Shirika la Afya Duniani (WHO) katika eneo la Mashariki ya Mediterania ametahadharisha kuhusu hali mbaya ya kiafya nchini Sudan kufuatia miapigano yanayoendelea baina ya makundi mawili ya jeshi la nchi hyo.
Maelfu ya wananchi wa Sudan wanakimbia mapigano yanayoendelea nchini humo leo yakiingia katika siku ya sita baada ya kugongwa mwamba jitihada za kusitisha mapigano. Hii ni mara ya pili ambapo usitishaji vita unakiukwa huko Sudan kati ya jeshi la taifana kundi lenye nguvu la wanajeshi wa Kikosi cha Radiamali ya Haraka (RSF).
Ripoti za vyombo vya habari zinaeleza kuwa mapigano yamezuka upya kati ya vikosi vya jeshi la Sudan vinavyoongozwa na Jenerali Abdel-Fattah al-Barhan na vikosi vya Radiamali ya Haraka RSF vinavyoongozwa na Mohammed Hamdan Daghlo maarufu kama Hamidati katika mji mkuu wa nchi hiyo Khartoum.
Takriban watu 185 wameuawa na wengine 1,800 kujeruhiwa katika mapigano ambaye yanaendelea kwa muda wa siku nne sasa kati ya pande zinazohasimiana nchini Sudan. Hayo ni kwa mujibu wa mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan huku jamii ya kimataifa ikitoa wito kwa pande hasimu kusitisha mapigano.
Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika liliitisha kikao cha dharura jana kujadiliana hali ya kisiasa na usalama nchini Sudan.
Mapigano makali yanaendelea katika mji mkuu wa Sudan, Khartoum, baada ya vita kuingia siku yake ya tatu, na zaidi ya watu 80 kuuliwa huku zaidi ya elfu moja wakijeruhiwa, kulingana na Shirika la Afya Duniani.
Nchini Sudan hali si shwari ambapo habari kutoka nchini humo zinaonyesha kuendelea mapigano kati ya jeshi la Sudan na vikosi vya radiamali ya haraka na kuzusha wasiwasi wa kutokea mapinduzi katika nchi hiyo ya Kiafrika.
Mapigano kati ya jeshi la Sudan na Vikosi vya Radiamali ya Haraka yameingia siku ya pili, huku milipuko ikisikika tangu alfajiri ya leo, Jumapili, karibu na Mji wa Michezo, kusini mwa mji mkuu, Khartoum.