Pars Today
Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Ethiopia amepuuza vitisho vya Misri na Sudan dhidi ya nchi hiyo na kusema kuwa, Cairo na Khartoum hazitaki kuona mzozo kuhusu Bwawa la al-Nahdha unapatiwa ufumbuzi na kumalizika.
Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Ethiopia amesema Sudan imeikabidhi nchi hiyo wakulima 59 na wanamgambo wawili wa kieneo.
Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Ethiopia amepinga mpango wowote wa kulifanya suala la bwawa la Renaissance kuwa mgogoro wa kimataifa.
Maafisa wawili wa Sudan wamefichua kuwa, ujumbe wa serikali ya nchi hiyo utafanya ziara ya kwanza rasmi kuelekea Israel (Palestina inayokaliwa kwa mabavu) wiki ijayo.
Wananchi wa Sudan wamefanya maandamano mbele ya ikulu ya rais wa nchi hiyo mjini Khartoum wakilalamikia hali mbaya ya uchumi na ughali wa maisha.
Mjumbe wa Baraza la Utawala wa Mpito nchini Sudan ametangaza kuwa, endapo nchi yake itaingia katika vita na Ethiopia basi itaibuka na ushindi.
Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Sudan amesema kuwa, ni jambo lililo mbali kwamba mgogoro wa bwawa la Renaissance unaweza kutatuliwa kwa njia za kijeshi ili kuizuia Ethiopia kuendeleza mradi ujenzi wa bwawa hilo juu ya maji ya Mto Nile.
Serikali ya Sudan imezungumzia tishio la kujazwa maji kenye bwawa la Renaissance lnalojengwa na Ethiopia juu ya maji ya Mto Nile na kusema kuwa, Khartoum itatumia nyenzo zote zinazowezekana kwa ajili ya kulinda raia wake.
Baraza la Mawaziri la Sudan limebatilisha sheria ya vikwazo na kuususia utawala wa Kizayuni wa Israel, miezi michache baada ya Khartoum na Tel Aviv kuafikiana juu ya kuanzisha uhusiano wa kawaida baina ya pande mbili hizo.
Kamati Kuu ya Madaktari wa Sudan imetangaza kuwa, watu wasiopungua 40 wameuawa katika mapigano ya kikabila yaliyotokea katika eneo la El-Geneina kwenye jimbo la Darfur, huko Magharibi mwa Sudan.