Makumi wauawa katika mapigano ya kikabila nchini Sudan
(last modified Tue, 06 Apr 2021 06:29:23 GMT )
Apr 06, 2021 06:29 UTC
  • Makumi wauawa katika mapigano ya kikabila nchini Sudan

Kamati Kuu ya Madaktari wa Sudan imetangaza kuwa, watu wasiopungua 40 wameuawa katika mapigano ya kikabila yaliyotokea katika eneo la El-Geneina kwenye jimbo la Darfur, huko Magharibi mwa Sudan.

Taarifa iliyotolewa na kamati hiyo imesema kuwa, watu wasiopungua 40 wameuawa na wengine 58 kujeruhiwa hadi sasa katika mapigano hayo yaliyoanza Jumamosi iliyopita.

Watu walioshuhudia pia wamesema kuwa, wanawake na watoto wadogo wamelazimika kukimbia makazi yao kutokana na mapigano hayo yanayoendelea hadi sasa. 

Jumatatu ya jana Baraza la Usalama wa Taifa la Sudan likiongozwa na Abdel Fattah al Burhan lilitangaza hali ya hatari katika jimbo la Darfur na kuliamuru Jeshi la Polisi kuchukua hatua zote za lazima ili kusitisha mapigano ya kikabila katika jimbo hilo. 

Waziri wa Ulinzi wa Sudan, Ibrahim Yassin amesema wizara hiyo imeunda kamati kuu ya kukabiliana na machafuko na ukiukaji wa mapatano ya amani huko El Geneina. 

Mapigano hayo yalianza Jumamosi iliyopita baada ya watu wawili wa kabila la Massalit kupigwa risasi na kuuawa na mahasimu wao.

Itakumbukwa kuwa tarehe 13 Januari makabila mawili ya Massalit na al Arab yalitia saini makubaliano ya kuhitimisha mapigano katika mji wa El Geneina. 

Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Uratibu wa Masuala ya Kibinadamu (OCHA) imesema kuwa, hali inabaki kuwa ya wasiwasi katika mji wa El-Geneina,      

Tags