Pars Today
Baada ya kutangazwa habari ya safari ya kwanza ya ujumbe wa utawala haramu wa Israel huko Khartoum, duru moja imethibitisha kufanyika mazungumzo baina ya ujumbe huo na viongozi wa serikali ya mpito ya Sudan.
Sudan imesusia kushiriki katika kikao cha mawaziri cha kujadili mradi wa bwawa la al Nahdha la nchini Ethiopia, ikiwa ni kulalamikia jinsi mazungumzo yanavyoendeshwa na nchi tatu za Ethiopia, Misri na Sudan.
Waziri wa Habari, Utamaduni na Utalii wa Sudan amefichua kuwa, Marekani iliiwekea nchi hiyo ya Kiafrika mashinikizo makubwa ya kuitaka ianzishe uhusiano na utawala haramu wa Israel.
Shirika la Wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR) limetangaza kuwa, vita vinavyoendela katika eneo la Tigray baina ya jeshi la serikali ya Ethiopia na wapiganaji wa Harakati ya Ukombozi wa Watu wa Tigray (TPLF) vimewalazimisha raia karibu elfu 30 kukimbilia nchi jirani ya Sudan.
Wizara ya Mambo ya Nje ya Sudan imekadhibisha taarifa kuwa ilifahamu juu ya safari ya ujumbe wa utawala haramu wa Israel katika mji mkuu wa nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika, Khartoum.
Majeshi ya Misri yametoa taarifa kuhusu mpango wa kufanyika luteka na mazoezi ya pamoja ya anga ya kijeshi kati ya nchi hiyo na Sudan katika anga ya Sudan.
Muungano wa vyama vya siasa vya Sudan vinavyopinga nchi hiyo kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni wa Israel umesema, upinzani wa wananchi kwa suala hilo ni mkubwa mno kwa kiwango ambacho haikukatarajiwa.
Mkuu wa Baraza la Utawala la Sudan ametangaza msamaha kwa watu wote waliokuwa wamebeba silaha kinyume cha sheria.
Serikali ya Russia imechapisha hati ya makubaliano yake ya Sudan yanayoiruhusu Moscow kujenga kambi ya kijeshi na misaada ya kilojestiki ya jeshi la majini la nchi hiyo nchini Sudan ambacho kitakuwa na askari na maafisa 300 wa kijeshi.
Kaimu waziri wa Afya wa Sudan Osama Ahmed Abdul Rahim pamoja na mkurugenzi mkuu wa huduma ya msingi ya afya na mkurugenzi mkuu msimamizi wa dawa za kimatibabu wa Wizara ya Afya wamepata ugonjwa wa COVIDI-19.