Waziri wa Afya wa Sudan aambukizwa COVID-19
(last modified Wed, 11 Nov 2020 07:59:07 GMT )
Nov 11, 2020 07:59 UTC
  • Waziri wa Afya wa Sudan aambukizwa COVID-19

Kaimu waziri wa Afya wa Sudan Osama Ahmed Abdul Rahim pamoja na mkurugenzi mkuu wa huduma ya msingi ya afya na mkurugenzi mkuu msimamizi wa dawa za kimatibabu wa Wizara ya Afya wamepata ugonjwa wa COVIDI-19.

Ikitoa taarifa Wizara ya Afya imesema watu hao walioathiriwa wanapatiwa matibabu na wapo kwenye hali nzuri, na kwamba waziri wa afya anaendelea na kazi zake akiwa kwenye kituo cha karantini.

Wakati huohuo, kamati ya juu ya dharura za afya nchini Sudan imewataka wananchi kupunguza mikusanyiko na safari katika kipindi cha sikukuu ili kukabiliana na kuenea kwa ugonjwa huo.

Sudan ina watu 707 walioambikizwa COVID-19 tangu mwanzoni mwa Novemba, idadi ambayo ni kubwa ikilinganishwa na mwanzoni mwa wimbi la kwanza.

Maabara ya kupima corona

Hadi sasa watu 14,155 wameambukizwa corona  nchini Sudan na wengine 1,116 wamefariki dunia. Maambukizi ya corona nchini Sudan yalianza kupanda tena wiki mbili zilizopita baada ya kushuka kwa wiki kdhaa.

 

 

Tags