-
Mazungumzo ya Wafghani yaendelea Doha, Taliban yakataa ombi la serikali la kusitisha vita
Sep 17, 2020 13:03Msemaji wa ofisi ya kisiasa ya kundi la Taliban nchini Qatar amelikataa ombi la serikali ya Afghanistan la kusitisha vita, wakati pande hizo mbili zinaendelea na mazungumzo ya amani katika mji mkuu wa Qatar, Doha.
-
Wafungwa waliosalia wa Taliban kuachiwa, mazungumzo ya amani ya Afghanistan kuanza wiki ijayo
Aug 28, 2020 11:50Wizara ya Mambo ya Nje ya Afghanistan imetangaza kuwa, karibuni hivi wafungwa waliosalia wa kundi la Taliban wataachiwa huru.
-
Sisitizo la Taliban la kufanya mazungumzo na serikali na makundi ya Kiafghani
Aug 18, 2020 00:27Kundi la Taliban nchini Afghanistan limetangaza kuwa mbali na serikali ya Kabul litafanya pia mazungumzo na makundi yote ya Kiafghani.
-
Jumamosi, 08 Agosti, 2020
Aug 08, 2020 04:23Leo ni Jumamosi tarehe 18 Mfunguo Tatu Dhul-Hija 1441 Hijria mwafaka na tarehe 8 Agosti 2020 Miladia.
-
Indhari ya Pompeo kwa Russia na madai ya kuondoka wanajeshi wa Marekani Afghanistan ifikapo Mei 2021
Aug 02, 2020 02:23Rais Donald Trump wa Marekani ameanzisha rasmi mchakato wa kuondoka wanajeshi wa nchi hiyo huko Afghanistan kabla ya wakati ulioainishwa awali, kwa kuzingatia ahadi alizotoa wakati wa kampeni za uchaguzi na mapatano iliyofikia Marekani na kundi la Taliban mwezi Februari mwaka huu. Hivi sasa Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Marekani anazungumzia kuainishwa wakati wa kukamilisha mchakato huo wa kuwaondoa wanajeshi wa nchi hiyo huko Afghanistan na wakati huo huo anatoa vitisho kwa Russia.
-
Serikali ya Afghanistan: Taliban katu haitashinda vita wala haitaidhibiti nchi
Jul 31, 2020 02:26Makamu wa Pili wa Rais wa Afghanistan amesisitiza kuwa, kundi la Taliban katu halitashinda katika vita vya nchi hiyo.
-
Baadhi ya wanamgambo wa Taliban walioachiwa huru kutoka jela wamerudi tena vitani
Jul 25, 2020 07:19Msemaji wa Baraza la Usalama wa Taifa la Afghanistan amesema wafungwa kadhaa wanamgambo wa kundi la Taliban ambao wameachiwa huru kutoka jela wamerudi tena kwenye medani za vita vya ndani vya nchi hiyo.
-
Taliban lakubali kwa masharti kuanza mazungumzo ya kutafuta suluhu na amani Afghanistan
Jul 24, 2020 07:36Kundi la Taliban limetangaza kuwa, liko tayari kwa masharti kuanza mazungumzo ya kutafuta suluhu na amani baina ya Waafghani.
-
Makamanda na wanamgambo 45 wa Taliban wauawa katika shambulio la anga la jeshi la Afghanistan
Jul 23, 2020 04:17Wanachama wasiopungua 45 wa kundi la Taliban wakiwemo makamanda na wanamgambo wa kundi hilo wameuawa katika shambulio la anga lililofanywa na jeshi la Afghanistan katika wilaya ya Adraskan jimboni Herat magharibi mwa nchi hiyo.
-
Araqchi akanusha madai ya kuwepo ofisi ya Taliban nchini Iran
Jul 19, 2020 14:36Naibu Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran anayehusika na masuala ya kisiasa amekabidhisha vikali madai ya kipropaganda kuwa kundi la wapiganaji wa Taliban la Afghanistan lina ofisi hapa nchini. Sayyid Abbas Araqchi aidha amekanusha vikali uvumi wa uwepo wa kundi la Taliban hapa nchini Iran, kwa jina la "Baraza la Mashhad."