-
Polisi visiwani Zanzibar yawaonya vikali wanasiasa 'wachochezi'
Oct 07, 2020 04:27Kamishna Mkuu wa Jeshi la Polisi Zanzibar nchini Tanzania amewatahadharisha wanasiasa dhidi ya kutoa matamshi ya kichochezi na uvunjifu wa amani visiwani humo, kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba 28.
-
Tume ya Uchaguzi Tanzania yamfungia Lissu kufanya kampeni
Oct 02, 2020 10:56Kamati ya Maadili ya Kitaifa ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi Tanzania (NEC) imemsimamisha mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, kufanya kampeni kwa muda wa siku saba, kwa madai ya kukiuka kanuni na taratibu za uchaguzi.
-
Magufuli asikitishwa na 'ajali' ya moto iliyoua wanafunzi 10 Tanzania
Sep 15, 2020 03:18Rais John Magufuli wa Tanzania ametuma salamu za rambirambi kwa uongozi wa Shule ya Kiislamu ya Byamungu iliyopo wilaya ya Kyerwa mkoani Kagera kufuatia mkasa wa moto uliosababisha maafa. Rais Magufuli ametoa mkono wa pole kwa wazazi, ndugu, jamaa na marafiki wa wanafunzi 10 waliopoteza maisha katika ajali hiyo ya usiku wa kuamkia jana.
-
Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania awasili Pemba kukabiliana na 'wachochezi'
Sep 04, 2020 02:33Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Tanzania Simon Sirro amewasili kisiwani Pemba, Zanzibar kwa ajili ya kile kilichotajwa kuwa kufanya vikao na vyama vya siasa na viongozi wa dini kuelekea uchaguzi mkuu wa mwezi ujao.
-
Msumbuji yachukua uwenyekiti wa SADC
Aug 17, 2020 23:07Tanzania imekabidhi Msumbiji uwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika, SADC huku jumuiya hiyo ikiadhimisha miaka 40 tangu kuasisiwa kwake.
-
Zoezi la kupiga kura uchaguzi mkuu Zanzibar kufanyika siku mbili
Aug 02, 2020 04:54Wananchi wa visiwa vya Zanzibar nchini Tanzania wanatarajiwa kupiga kura kwa siku mbili katika uchaguzi mkuu utakafanyika Oktoba mwaka huu.
-
Tanzania yazuia safari za Kenya Airways nchini humo
Jul 31, 2020 23:33Tanzania imesimamisha shirika la ndege la Kenya (KQ) kufanya safari za kwenda Tanzania kuanzia leo tarehe Mosi Agosti, siku moja baada ya Kenya kutangaza kuwa itafungua anga zake kwa usafiri wa kimataifa isipokuwa kutoka baadhi ya nchi ikiwemo Tanzania.
-
Rais mstaafu wa Tanzania, Benjamin Mkapa, anazikwa leo
Jul 29, 2020 03:10Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Benjamin William Mkapa anazikwa leo katika kijiji alichozaliwa cha Lupaso katika Wilaya ya Masasi, mkoa wa Mtwara Kusini mwa nchi hiyo.
-
Lissu awasili Tanzania, apokewa na wafuasi na viongozi wa Chadema
Jul 27, 2020 08:35Mwanasheria na mwanasiasa mashuhuri wa kambi ya upinzani nchini Tanzania Tundu Antipas Lissu amewasili nchini humo baada ya kuwa nje ya nchi kwa matibabu kwa zaidi ya miaka miwili, baada ya kunusurika kifo kwa shambulio la risasi akiwa Dodoma.
-
Majaliwa: Mwili wa Mkapa kuagwa Uwanja wa Taifa, Kenya yatuma salamu za rambirambi
Jul 24, 2020 06:41Waziri Mkuu wa Tanzania ametangaza kuwa mwili wa rais wa zamani wa nchi hiyo, Benjamin Mkapa aliyeaga dunia mapema leo, utaagwa Uwanja wa Taifa na kwamba siku ya kuuaga itatangazwa hapo baadaye.