-
Viongozi wa dini Tanzania: Kubeti ni kamari, ni haramu! + Sauti
Jan 27, 2019 14:50Viongozi wa kidini na wa kiserikali nchini Tanzania wamekemea vitendo vya kubeti na kucheza kamari ambavyo vimekithiri nchini humo hali ambayo inapelekea kuzalika vijana wasiofanya kazi wakiweka matumaini zaidi ya kupata kipato chao kupitia njia hizo. Ammar Dachi na maelezo zaidi kutoka Dar es Salaam Tanzania.
-
Burundi: Kuna njama za kuvuruga uhusiano wetu na Tanzania + Sauti
Jan 21, 2019 14:51Mashirika ya Capes na Pisc ya nchini Burundi yamesema kuwa, kugunduliwa sare za jeshi la Tanzania katika kambi ya wakimbizi huko Burundi kunadhihirisha kuwepo njama za kutaka kuvuruga uhusiano mzuri uliopo kati ya nchi hizo mbili. Hamida Issa na maelezo zaidi kutoka Bujumbura.
-
CAG Tanzania ahojiwa na kamati ya bunge, huku Mahakama Kuu ikipokea kesi ya kupinga kuhojiwa kwake
Jan 21, 2019 13:03Kamati ya Maadili, Haki na Madaraka ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imemuhoji Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad kuhusu kauli yake ya “udhaifu wa Bunge la nchi hiyo.”
-
SAUTI, Ripoti ya matukio ya Kiislamu, Waislamu Tanzania walaani hatua ya kuvunjwa msikiti wa Chuo Kikuu Dodoma/ Waislamu Kenya walaani ugaidi
Jan 18, 2019 13:12Wanaharakati na watetezi wa haki za binaadamu nchini Tanzania wamelaani vikali kitendo cha Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma, Dodoma, Petter Msoffe kusimamisha ujenzi wa msikiti chuoni hapo na kukitaja kitendo hicho kuwa kinakiuka haki ya binaadamu na uhuru wa kuabudu.
-
Rais Magufuli: Ni vigumu changamoto zilizosalia nchini Tanzania kupata wa kuzitatua baada yangu
Jan 18, 2019 12:42Rais John Pombe Magufuli wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amesema kuwa, kama kuna changamoto ambazo bado hazijafanyiwa kazi katika uongozi wake, basi hana uhakika iwapo kiongozi atakayekuja baada yake atakuwa na uwezo wa kuzitatua.
-
Zitto Kabwe aufikisha mgogoro wa Spika wa Bunge la Tanzania na CAG katika ngazi ya kimataifa
Jan 10, 2019 12:28Mgogoro ulioibuka kati ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad, umezidi kuwa mkubwa baada ya kiongozi wa chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Zuberi Kabwe kumuandikia barua Katibu Mkuu wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola (CPA), Akbar Khan akimtaka kuingilia kat.
-
Mufti wa Tanzania ataka mahujaji wa nchi hiyo watumie Air Tanzania + Sauti
Jan 05, 2019 02:50Viongozi wanaosimamia misafara ya Hija nchini Tanzania wametakiwa kutumia ndege za Shirika la Ndege la Air Tanzania katika msimu wa Hija kama njia ya kuunga mkono jitihada za rais wa nchi hiyo za kuliletea maendeleo Taifa. Ammari Dachi na ripoti kamili kutoka Dar es Salaam.
-
Msumbiji: Raia wa Tanzania na Afrika Kusini ndio wanaoongoza 'al-Shabaab'
Jan 01, 2019 04:46Waendesha Mashitaka nchini Msumbiji wamewataja raia wawili wa Tanzania na mmoja wa Afrika Kusini kuwa miongoni mwa makamanda wa kundi la kigaidi la al-Shabaab ambalo hapo awali lililikuwa linajiita Ahlu Sunna Wal Jamaa, linalofanya hujuma za umwagaji damu katika mkoa wa Cabo Delgado, kaskazini mwa nchi.
-
Wahajiri 14 wa Ethiopia waaga dunia katika mazingira ya kutatanisha Tanzania
Jan 01, 2019 04:42Polisi ya Tanzania imetangaza habari ya kuaga dunia wahamiaji 14 waliothibitishwa kuwa raia wa Ethiopia mkoani Morogoro, mashariki mwa Tanzania.
-
Kamati ya amani Tanzania inayojumuisha Waislamu na Wakristo yaadhimisha mazazi ya Nabii Isa AS + Sauti
Dec 29, 2018 14:57Kamati ya amani nchini Tanzania ambayo inajumuisha viongozi wa Kiislamu na Kikristo wa madhehebu mbalimbali, imefanya sherehe maalumu za kuadhimisha mazazi ya Nabii Isa AS na mwaka mpya wa Milaadia. Maelezo zaidi yamo kwenye ripoti ya mwandishi wetu Ammar Dachi...