-
Serikali ya Tanzania yalalamikiwa kwa kuvunja ahadi iliyotoa kwa Waislamu
Sep 28, 2023 11:45Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini Tanzania zimeilalamikia Serikali ya nchi hiyo kwa kuvunja ahadi yake ya kuwapa umiliki wa mitaala ya somo la elimu ya dini ya kiislamu.
-
Kuongezeka mabadilishano ya kibiashara kati ya Iran na Tanzania
Sep 17, 2023 10:30Mkuu wa Kituo cha Biashara cha Iran na Tanzania amesema kuwa, kufanyika maonyesho ya kwanza ya kipekee ya uwezo wa usafirishaji wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Tanzania kuwa jukwaa linalofaa zaidi la kuongeza ufahamu wa bidhaa za Iran katika nchi za Afrika Mashariki.
-
Sheikh Ponda: Wanawake Waislamu Tanzania washiriki katika masuala ya kitaifa
Sep 16, 2023 07:24Katibu wa Shura ya Maimamu nchini Tanzania Sheikh Ponda Issa Ponda amewataka wanawake wa Kiislamu nchini humo washiriki katika masuala ya kitaifa ikiwemo masuala ya maendeleo na uongozi na kutahadharisha kuwa kutofanya hivyo kunatoa nafasi kwa watu wengine kushiriki kwa niaba yao.
-
Wafanyakazi Waturuki wanaojenga reli ya SGR Tanzania wagoma baada ya mishahara kucheleweshwa
Aug 12, 2023 23:10Mamia ya wafanyakazi Waturuki walioajiriwa na kampuni ya ujenzi ya Uturuki ya Yapı Merkezi katika mradi wa reli ya Tanzania ya Standard Gauge (SGR) wamegoma tangu Agosti 5, wakitaka kulipwa mishahara yao ambayo hawajalipwa kwa muda wa miezi saba iliyopita.
-
IGP wa Tanzania atoa onyo kali kwa wanaochochea maandamano kwa lengo la kuipindua Serikali
Aug 11, 2023 09:42Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania IGP Camillus Wambura amesema, kuna kundi la watu ambao wamepanga kuandaa maandamano nchi nzima ili kuiangusha Serikali ya Jamhuri ya Muungano ya awamu ya sita kabla ya mwaka 2025.
-
Vyama Tanzania vyataka CHADEMA ifutiwe usajili kwa kuchochea udini na kutusi viongozi
Aug 02, 2023 04:29Baadhi ya vyama vya siasa vya upinzani nchini Tanzania vimeitaka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa ya nchi hiyo ivifutie usajili vyama vinavyokiuka sheria katika ufanyaji mikutano ya hadhara, kwa kutoa lugha za kuchochea ubaguzi, udini na kejeli dhidi ya viongozi wa serikali.
-
Baraza la Vyama vya Siasa Tanzania lafanya mkutano wa dharura kujadili hali tete ya kisiasa nchini
Aug 01, 2023 09:59Baraza la Vyama vya Siasa nchini Tanzania limefanya mkutano wa dharura kwa lengo la kujadili hali ya kisiasa nchini humo.
-
Serikali ya Tanzania yaweka pingamizi kesi ya kupinga uwekezaji bandarini
Jul 17, 2023 08:40Serikali ya Tanzania imeweka mapingamizi katika kesi iliyofunguliwa na mawakili wanne kupinga uwekezaji wa bandari za nchi hiyo na kuitaka Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya iitupilie mbali kwa madai kwamba iko kinyume cha sheria na Katiba ya nchi.
-
Viongozi wa Afrika wajadili njia za kupunguza rushwa barani humo
Jul 09, 2023 08:38Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar nchini Tanzania, Hemed Suleman Abdulla amezitaka nchi mbalimbali barani Afrika kushirikiana na kushikamana ili kupunguza vitendo vya rushwa barani humo.
-
Ukatili wa kingono CAR; UN kuwatimua askari 60 wa Tanzania
Jun 10, 2023 07:52Umoja wa Mataifa umesema utawafukuza makumi ya askari wa Tanzania, ambao ni sehemu ya Kikosi cha Kulinda Amani cha moja huo nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati (MINUSCA) kwa kutuhumiwa kufanya unyanyasaji wa kingono.