-
Askari wa Tanzania, Botswana wauawa Cabo Delgado, Msumbiji
Dec 02, 2022 02:44Wanajeshi wawili wa kikosi cha Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika SADC wameuawa katika makabiliano baina yao na wanamgambo katika jimbo la Cabo Delgado kaskazini mwa Msumbiji.
-
Viongozi wa Tanzania watakiwa kutoa uhuru wa kisiasa + SAUTI
Nov 21, 2022 02:21Viongozi Wakuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wametakiwa kuhakikisha harakati za kisiasa zinafanyika katika mazingira ya uhuru na haki nchini humo. Harith Subeit na maelezo zaidi kutoka Zanzibar.
-
Nchi za Afrika zakutana Zanzibar kujadili maji safi na taka
Nov 15, 2022 07:51Nchi 42 za Afrika zinakutana Zanzibar nchini Tanzania kuanzia leo kujadili na kubadilishana uzoefu kuhusu udhibiti wa sekta ya maji safi na taka Afrika.
-
Mabaharia 16 Wairani waachiliwa huru Tanzania
Nov 13, 2022 04:46Mabaharia 16 Wairani waliokuwa wanashikiliwa nchini Tanzania wameachiliwa huru hivi karibuni. Hayo yamedokezwa na Mkuu wa Ofisi ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran katika Eneo la Biashara Huria la Chabahar katika mkoa wa Sistan na Baluchestan kusini-mashariki mwa Iran ambaye amesema mabaharia hao walioachiliwa huru ni wenyeji wa mkoa wa Sistan na Baluchestan.
-
Walimu waliombadilishia namba ya mtihani mwanafunzi wa Darasa la 7 Tanzania wafukuzwa kazi
Oct 26, 2022 02:33Serikali ya Tanzania imeifungia Shule ya Awali na Msingi ya Chalinze Modern Islamic kuwa kituo cha Mitihani pamoja na kuwafuta kazi wasimamizi wa mtihani ambao ni walimu kutokana na udanganyifu uliofanyika katika Mtihani wa Darsa la Saba uliofanyika tarehe 5 na 6 za mwezi huu wa Oktoba.
-
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran apongeza kuteuliwa mwenzake wa Tanzania
Oct 18, 2022 07:54Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amemnyooshea mkono wa tahania Stergomena Lawrence Tax, kwa kuteuliwa kuwa Waziri mpya wa Mashauri ya Kigeni wa Tanzania.
-
Daktari Mtanzania aaga dunia kwa Ebola nchini Uganda
Oct 01, 2022 12:14Daktari mmoja raia wa Tanzania aliyekuwa akifanya kazi nchini Uganda ameaga dunia kutoka na ugonjwa wa Ebola.
-
Maadhimisho ya Arubaini ya Imam Hussein yafanyika Tanzania, Nigeria, Niger
Sep 18, 2022 08:16Waislamu ya madhehebu ya Shia Tanzania, visiwani Zanzibar, Nigeria na Niger wamefanya marasimu, matembezi na vikao vya kuadhimisha Arubaini ya Imam Hussein (AS).
-
Mkuu wa UNHCR awataka wahisani waisaidie Tanzania kwa inavyoendelea kukirimu wakimbizi
Aug 28, 2022 07:07Kamishna Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi UNHCR amewahimiza wahisani kuunga mkono zaidi suluhu na hiari juu ya suala la wakimbizi na kusifu maendeleo yaliyopigwa katika ulinzi wa wakimbizi nchini Tanzania.
-
Iran: Uhusiano wetu na Tanzania unazidi kustawi na kuimarika
Aug 27, 2022 11:51Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter kuwa, uhusiano wa Tehran na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania unazidi kuwa imara.