-
Guterres: Afrika ina mchango muhimu kwa amani na usalama wa dunia
May 24, 2024 03:52Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameashiria nafasi muhimu ya Afrika katika kuufanya ulimwengu uwe pahala pazuri na salama na kusisitiza kuwa, "Wakati umefika wa kuanika uwezo wa amani wa Afrika."
-
TZ yaitoa hofu UNHCR: Hatutafunga kambi wala kuwalazimisha wakimbizi warudi makwao
May 23, 2024 03:49Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi UNHCR limesema limepewa hakikisho na Serikali ya Tanzania kwamba kambi ya wakimbizi ya Nduta inayowapa hifadhi wakimbizi wa Burundi haitafungwa na wala wakimbizi hao hawatalazimishwa kurudi makwao.
-
UN: 40% ya wakazi wa Gaza wamelazimika kuhama makwao ndani ya wiki 2
May 21, 2024 03:49Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadu (OCHA) imesema asilimia 40 wa Wapalestina wa Ukanda wa Gaza wamelazimika kuyahama makazi yao katika kipindi cha wiki mbili zilizopita.
-
OCHA: Kwa kuzuiwa uingizaji misaada, hakuna kilichobaki kugawa katika Ukanda wa Ghaza
May 18, 2024 23:18Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Uratibu wa Masuala ya Kibinadamu (OCHA) imeonya dhidi ya kuzuiwa uingizaji misaada ya kibinadamu katika Ukanda wa Ghaza na kutangaza kuwa hakuna kilichosalia kwa ajili ya kuwagaia Wapalestina wa eneo hilo.
-
Katibu Mkuu wa UN alaani mauaji ya wafanyakazi wa afya huko Rafah
May 15, 2024 03:26Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, amelaani mauaji na kujeruhiwa kwa maafisa wa afya wa Umoja wa Mataifa huko Rafah kusini mwa ukanda wa Gaza.
-
Kuidhinishwa rasimu ya uanachama kamili wa Palestina katika Umoja wa Mataifa
May 11, 2024 07:51Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA) hatimaye limeipigia kura ya ndio rasimu ya uanachama kamili wa Palestina katika umoja huo baada ya Marekani kukwamisha suala hilo kwa miaka kadhaa.
-
Iravani: Madai ya uwongo ya Israel dhidi ya Iran; juhudi za kuupotosha ulimwengu kuhusu jinai za Gaza
May 02, 2024 04:13Mwakilishi wa Kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa ameyataja madai ya uwongo ya Israel dhidi ya Iran kuwa ni juhudi zenye lengo la kupotosha mazingatio ya walimwengu kuhusu jinai za utawala wa Kizayuni dhidi ya watu wa Ukanda wa Gaza.
-
Mahakama ya UN yatoa waranti wa kukamatwa rais wa zamani wa Jamhuri ya Afrika ya Kati
May 01, 2024 07:22Mahakama Maalumu ya Jinai (CPS) inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa imesema, imetoa hati ya kukamatwa Rais wa zamani wa Jamhuri ya Afrika ya Kati Francois Bozize kwa tuhuma za kuhusika na uhalifu dhidi ya binadamu unaodaiwa kufanywa na jeshi wakati wa uongozi wake.
-
UN: Ukatili wa polisi ya Marekani dhidi ya watetezi wa Palestina unatia wasiwasi
May 01, 2024 03:49Kamishna Mkuu wa Haki za Kibinadamu wa Umoja wa Mataifa ameelezea wasiwasi wake juu ya unyanyasaji wa polisi wa Marekani dhidi ya wanafunzi wanaoiunga mkono Palestina.
-
UN: Kombora la balestiki la Korea Kaskazini limetumika kushambulia mji wa Kharkiv, Ukraine
Apr 30, 2024 03:51Wachunguzi wa vikwazo wa Umoja wa Mataifa wameiambia kamati ya vikwazo ya Baraza la Usalama la umoja huo kuwa, mabaki ya kombora yaliyopatikana katika mji wa Kharkiv nchini Ukraine mnamo Januari 2 yanatokana na kombora la balestiki la Korea Kaskazini aina ya Hwasong-11.