May 24, 2024 07:22 UTC
  • Guterres: Afrika ina mchango muhimu kwa amani na usalama wa dunia

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameashiria nafasi muhimu ya Afrika katika kuufanya ulimwengu uwe pahala pazuri na salama na kusisitiza kuwa, "Wakati umefika wa kuanika uwezo wa amani wa Afrika."

Antonio Guterres, Katibu Mkuu wa UN alisema hayo jana Alkhamisi akihutubia kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa cha kujadili mchango wa nchi za Afrika kwa amani na usalama wa dunia.

Amesema, "Kwanza, tunahitaji amani barani Afrika kwenyewe, na pili, tunapaswa kuimarisha nafasi na ushiriki wa Afrika kwenye mchakato wa amani na usalama wa dunia."  

Guterres amesema ana wasiwasi mkubwa kufuatia mapigano ya karibuni kati ya jeshi la Sudan na wanamgambo wapinzani katika mji muhimu wa Darfur wa El-Fasher nchini humo.

Kustawi uchumi wa Afrika

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ametaka kusitishwa vita haraka iwezekanavyo na kuzitolea wito pande zote husika kuwaruhusu raia kuelelea katika maeneo salama na kuwezesha huduma za kibinadamu. 

Kadhalika Guterres amesema nchi nyingi za Afrika zinajaribu kujikwamua kutoka kwenye minyororo ya ukoloni na kwamba, "Tangu wakati huo (enzi za ukoloni), dunia imebadilika, lakini taasisi za kimataifa hazijabadilika."

Tags